Meneja Ugawaji wa huduma za TBL Group,James Nyoike,amesema
kuwa utumiaji wa vifaa bora na vya kisasa unapunguza matukio ya
ajali sehemu za kazi hususani viwandani na kuongeza ufanisi wa kazi
na kuongeza uzalishaji.
Bw.Nyoike aliyasema hayo wakati wa kupokea magari ya kupakia na kupakua
mizigo (Forklifts) za kisasa zilizonunuliwa na kampuni hiyo kutoka
kampuni ya kusambaza vifaa vya viwandani ya Effco Solution Limited.
Alisema kampuni ya TBL Group inao makakati kuhakikisha
inatumia mitambo ya kisasa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kulinda
usalama wa wafanyakazi wake ikiwemo kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji
“Tunapoongelea vifaa vya kisasa hatumaanishi mitambo tu bali hata vifaa vyote
vinavyotumika katika kazi ikiwemo magari yanaotumika kusambaza bidhaa zetu na
yanaotumiwa na wafanyakazi wetu katika shughuli mbalimbali
“.Alisema.
Dereva akiendesha moja ya Forklift nne za kisasa zilizonuliwa na
kampuni
Meneja Ugavi na Usambazaji wa TBL Group ,James Nyoike
( wa Nne kutoka kulia) na madereva wa kuendesha Forklifts
wakimsikiliza mtaalamu kutoka EFFCO Solution Donald
Luvaga (kushoto), jinsi Forklift za kisasa aina ya Toyota zilizonunuliwa
na kampuni ya TBL zinavyofanya kazi.
Mtaalamu kutoka EFFCO Solution, Donald
Luvaga kitoa maelekezo kwa Madereva wa Forklift wa TBL Group.
0 comments:
Post a Comment