Zoezi la uchangiaji Damu likiendelea katika makao makuu ya TAZARA
ambapo wafanyakazi mbalimbali wa Shirika hilo na watanzania wengine
wamejitokeza kucnagia damu Wakati Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia TAZARA
Wakiadhimisha miaka 40 ya uwepo wake nchini Tanzania maadhimisho hayo yameenda sambamba na zoezi maalum la kuchangia damu zoezi ambalo limefanyika makao makuu ya TAZARA Dar es salaam Tanzania ambapo wafanyakazi wake wameitumia siku ya leo kuchangia damu zoezi ambalo liliongozwa na mpango wa Taifa wa damu salama Tanzania.
wafanyakazi wa TAZARA wakiwawanachangia damu
Akizungumza na wanahabari
wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU
amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa Damu uliopo Tanzania wao kama TAZARA
wameamua kusitisha shughuli za leo kwa ajili ya kufanya zoezi moja la kuchagia
damu zoezi ambalo linaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwake.
Aidha mmoja kati ya
wahamashishaji kutoka mpango wa taifa wa Damu salama Tanzania Bi Mariam Juma
amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhitaji mkubwa damu kutokana na kuongezeka kwa
maswala mbalimbali yakiwemo ya ajali,vifo vya mama na watoto wakati wa
kujifungua wanaofariki kwa kukosa damu,na magonjwa mengine mengi hivyo
akawataka watanzania kujitahidi na kuhakikisha kuwa angalau wanachangia damu
kwa mwaka japo mara mbili ili kuokoa maisha ya watanzania wenzao.
Wafanyakazi wa TAZARA walijitokeza kwa wingi
kuchangia Damu ambapo walimueleza mwandishi wetu kuwa ni swala la kizalendo na
utu kwa mtanzania kujali na kusaidia watanzania wengine ambao wana uhitaji
mkubwa wa damu nchini.Source:Habari24 Blog
Mkurugenzi mtendaji wa Tazara
ENG BRUNO TANDU CHINGANDU akizngumza na wanahabari wakati wakiendelea na zoezi
la ucnagiaji wa Damu
Amesema kuwa zoezi hilo linaonyesha
ni jinsi gani wafanyakazi wa TAZARA wamekuwa wakiguswa na maswala mbalimbali ya
kijamii hususani swala la ukosefu wa Damu mahospitalini huku akiyataka
mashirika mengine na watu mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachangia damu mara kwa
mara wawezavyo kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wamaopoteza maisha yao
kwa kukosa Damu.
Mmoja kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa Taifa wa Damu salama
Tanzania Bi Mariam Juma akifafanua jambo juu ya umuhimu wa kucnagia Damu kwa
watanzania
0 comments:
Post a Comment