Nafasi Ya Matangazo

August 03, 2016

Afisa Masoko na Utafiti Mkuu wa AICC Bi.Linda Nyanda akitoa maelezo kuhusiana na huduma zitolewazo na AICC na JNICC kwa Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi SACP Tusekile Mwaisabila akiwa ameambatana na RSO wa Mkoa wa Lindi.
*******

Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) kimeshiriki maonesho ya Nane nane yanayofanyika kitaifa viwanja vya Ngongo, Mkoa wa Lindi. Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Sospeter Muhongo yakiwa na kauli mbiu “Kilimo, mifugo na uvuvi ni nguzo ya maendeleo. Kijana shiriki kikamilifu.

Kupitia maonesha ya Nane Nane mwaka huu AICC pamoja na tawi lake la Dar es Salaam, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) inapata fursa ya kukutana na wadau wake na wananchi kwa ujumla kuwaelezea juu ya huduma zitolewazo na Shirika hilo. Huduma hizo ni pamoja na utalii wa mikutano, upangishaji wa nyumba za makazi na nafasi za ofisi kwa upande wa Arusha.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Bw.Jomaary M. Saturi akisikiliza kwa makini maelezo toka kwa Mkuu wa Masoko na Utafiti wa AICC Bi.Linda Nyanda, alipotembelea banda la AICC kwenye maonesho ya Nane nane yanayoendelea Mkoani Lindi
Posted by MROKI On Wednesday, August 03, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo