Mkurugenzi
Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali Bi. Sarah Mwaipopo akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za
Kiraia wakati wa ufunguzi wa kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali
wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za
binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za
binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe
kutoka Serikalini na Asasi mbalimbali za Kiraia wakimsikiliza Mkurugenzi
Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali Bi. Sarah Mwaipopo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili
mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi
ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa
kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi Masuala ya Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Bi. Nkasori Sarakikya akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi mbalimbali
za Kiraia mara baada ya ufunguzi wa kikao cha kujadili mapendekezo yaliyotolewa
kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala
ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la
haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni
Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi hiyo Bi. Sarah
Mwaipopo.
Mjumbe
kutoka Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Bi.
Blandina Sembu akichangia hoja kwenye eneo la watu wenye ulemavu na masuala ya
uandishi wa Habari wakati wa kikao cha kujadili mapendekezo yaliyotolewa kwa
serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya
haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki
za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam. Na Hassan Silayo-MAELEZO. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Serikali,kupitia Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo imefanya
kikao maalumu cha wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na asasi
za kiraia kwa lengo la kuwafahamisha kuhusu kujadiliwa kwa Taarifa ya pili ya
nchi ya utekelezaji wa masuala ya Haki za Binadamu chini ya mfumo wa mapitio
kwa kipindi maalum (The Universal Period Review).
Vilevile kikao hicho kitatoa fursa
ya kujadili kwa kina na kuyapatia misismamo ya awali kama wadau, mapendekezo yaliyotolewa
na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa Serikali mnamo mwezi Mei
2016 , na kuainisha sababu ambazo zinafaa kwa mapendekezo yaliyoahirishwa kwa
maslahi mapana ya nchi yetu kabla ya kupitishwa rasmi kuwa taarifa ya nchi itakayowasilishwa kwenye
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kabla ya terehe 9 Septemba 2016.
Akifungua kikao hicho Mkurugenzi wa
masuala ya Katiba na Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa
Serikali, Bi Sarah Mwaipopo ameeleza kuwa kikao hicho ni hatua muhimu kkatika mfumo
wa maandalizi ya taarifa za usimamizi na utekelezaji wa haki za binadamu nchini
ambao umekua ukishirikisha wadau wote kutoka Wizara,Idara na Taasisi za
Serikali pamoja na Taasisi zisizo za kiserikali ambapo amesisitiza wadau wote
kuendelea kutoa ushirikiano na kutimiza
wajibu wao ipasavyo.
“Sote
tutambue na kuzingatia kwamba masuala ya haki za biandamu ni mtambuka na kila
mtu ana wajibu wa kutekeleza na kuyasemea katika eneo lake”alisema Bi Sarah
Halikadhalika,kwa niaba ya Serikali,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekua ikiratibu kikamilifu
maandalizi na uwasilishwaji wa Taarifa
zote za masuala yote ya haki za
binadamu kwa kuzingatia mikataba ya Haki za Binadamu ambayo Tanzania imeridhia
na utekelezaji wa jukumu hili umeanishwa katika Ibara ya 59(3) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Sura ya 268, kifungu cha 14(f) ambayo ni;
kuratibu masuala ya uaandaaji na utoaji wa
taarifa za nchi za utekelezaji wa Mikataba ya Kikanda na Kimataifa ya haki za
binadamu amabyo nchi imeridhia ikiwemo masuala yote ambayo yanahitaji utolewaji
wa taarifa za aina hiyo na kuziwasilisha kwenye vyombo husika vya Kikanda na Kimataifa
kwa ajili ya majadiliano.
Kikao hicho ambacho kitafanyika
kuanzia tarehe 30 -31 Septemba 2016 jijini Dar es Salaam kimehudhuriwa na wadau
kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao ni
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jukwaa la Katiba Tanzania,Chama
cha Watu wenye Ualbino Tanzania,MISA-TAN,PINGOS’ FORUM,Ofisi ya Msajili wa
Vyama vya Siasa,Wizara ya Katiba na Sheria, Mahakama ya Tanzania,Uhamiaji,Tume
ya Haki za Binadamu na utawala bora, Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA),
Shrikisho la Watu wenye ulemavu Tanzania( SHIVYAWATA) na Msajili wa Mashirika
yasiyo ya Kiserikali. Kwa upande wa Zanzibar ni Wizara ya Kilmo na Mifugo,
Wizara za Afya,Mifugo, Kazi,Vijana Wazee,Ofisi ya Mwansheria Mkuu, Jumuia ya
Wanawake Wanasheria,Tume ya Uchaguzi
Utaratibu wa Mapitio kwa kipindi
maalum (The Universal Periodic Review) wa masuala ya haki za binadamu
ulianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2006 kwa lengo la kuzifanyia
mapitio nchi 192 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania ikiwa miongoni,
kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa masuala ya kulinda na kukuza haki za
binadamu nchini mwao.
0 comments:
Post a Comment