WATU zaidi ya saba wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya CRDB tawi la Mbande, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam na kuwauwa kwa risasi Askari Polisi wanne na kujeruhi raia wawili.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba pamoja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro walitembelea eneo la tukio jana usiku na kuwajulia hali majeruhi hao.
"Usiku huu nimefika Mbande-Temeke,eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya CRDB-Mbande na kuua askari 4 waliokuwa wakishuka kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo," alisema Mwigulu.
Pia Waziri Mwigulu aliwatembelea mejeruhi hao wawili na kusema hali zao zinaendelea vyema.
Mwigulu alitoa wito kwa raia kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kuwafichua wahalifu hao lakini pia aliwataka wale walioshiriki kujisalimisha mara moja.
"Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa rai kwa wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu," alisema Mwigulu.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba (aliyevalia sare za polisi kushoto) akioneshwa eneo la tukio na gari walilokua wakilitumia Polisi hao.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akienda kuangalia tukio hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akimjulia hali mmoja wa majeruhi wa tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment