Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili
kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja wa ujumbe wa Shirika la Kimataifa lisilo la
Kiserikali la Global Communities uliomtembelea leo ofisini kwake Ikulu jijini
Dar es Salaam wengine pichani ni kutoka kushoto ni Meneja wa Biashara Ndugu
Lucas Mazige,Meneja wa Shirika hilo Ndugu Mwita Mchuni , kulia ni Meneja
wa Mikopo wa Shirika hilo Ndugu Victor Anthony .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka kampuni ya MER GROUP,wa kwanza kushoto ni Meneja wa Kampuni hiyo Bw. Dov Aronovich, wengine ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Omer Leviv na Meneja wa Biashara Bw. Mohammed Magori, Ujumbe huu ulimtembelea Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam na kutambulisha shughuli wanazofanya nchini.
**********
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka kampuni ya MER GROUP,wa kwanza kushoto ni Meneja wa Kampuni hiyo Bw. Dov Aronovich, wengine ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Omer Leviv na Meneja wa Biashara Bw. Mohammed Magori, Ujumbe huu ulimtembelea Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam na kutambulisha shughuli wanazofanya nchini.
**********
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameutaka
uongozi wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la Global Communities
uhakikishe unaweka utaratibu bora wa kupata taarifa muhimu kuhusu masuala ya
kilimo kutoka kwa wakulima wenyewe hatua ambayo itasaidia serikali, wafadhili
na wadau wengine wa maendeleo kukipa msukumo wa kipekee kilimo ili kiweze kuwa
na tija nchini.
Makamu
wa Rais ametoa kauli hiyo 17-Aug-16 alipokutana na ujumbe wa watu watatu wa
shirika hilo ukiongozwa na Programu Meneja Mwita Mchumi ambao ulimtembelea
ofisini kwake Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha na kuelezea shughuli
zinazofanywa shirika hilo nchini.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa kama wakulima wakipata taarifa sahihi kuhusu masuala
ya kilimo na masoko wataweza kuongeza uzalishaji wa mazao na hivyo kuleta
mapinduzi makubwa ya kilimo kwa kujiongezea kipato na la taifa kwa ujumla.
"Changamoto
kubwa katika kilimo ni hii ya kukosekana kwa taarifa kutoka kwa wakulima
wenyewe. Nyinyi kama shirika wekeni kama mradi hivi, mnaenda mfano Singida
mnaongea na wakulima wenyewe aina ya mazao ya biashara yanayolimwa pale,
pembejeo wanapata kwa wakati na inakidhi haja vitu kama hivyo. Taarifa hizo
zitaisadia serikali, wafadhili kukiwezesha kilimo kuwa na tija," alisema
Mheshimiwa Samia.
Katika
mazungumzo hayo Mwita Mchumi aliiomba serikali iangalie uwezekano wa kupunguza
riba ili kuwawezesha wafanyabiashara na wakulima kukopa kwenye mabenki jambo ambalo Makamu wa Rais alisema serikali
inalifanyia kazi.
Shirika
la Global Communities lenye makao yake makuu Washington, Marekani tangu
lilipoanza kazi rasmi hapa nchini mwezi Februari mwaka huu limeweza kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi
wadogo na wa kati wa biashara za kilimo ambao wameweza kufanya biashara ya
takribani Dola za Kimarekani milioni 150.
Shirika
hilo limeweza pia kufundisha mabenki umuhimu wa mfumo wa kuuza mazao
kupitia stakabadhi ghalani na kuifanya
Benki ya Afrika (BOA) kutenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuwakopesha
wakulima wadogo wadogo wanaojishughulisha kuuza mazao kupitia stakadhi ghalani
katika mkoa wa mbeya
Kwa
mujibu wa Mwita Mchumi hivi sasa kuna mafunzo yanaendelea ngazi ya cheti katika
kuwajengea uwezo wataalam wa benki katika biashara za kilimo ili waweze kutoa
huduma stahiki katika sekta ya kilimo.
Mwita
Mchumi amesema shirika hilo ambalo limeanzishwa mwaka jana linajishughulisha zaidi na masuala ya kilimo
hasa biashara za kilimo katika minyororo ya thamani ya mazao ya nafaka, jamii
ya mikunde, bustani, mifugo na mazao ya mafuta kama alizeti na ufuta.
Shirika
hilo pia linatumia njia za tehama katika kupata taarifa za masoko na
kuwakutanisha wauzaji kwa ajili ya kuingia biashara na kujenga uwezo kwa
wafanyabiashara wa kati na wadogo pamoja na wakopeshaji ambao ni taasisi za
kifedha kama mabenki.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
0 comments:
Post a Comment