Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji
Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika.
Rais wa Chama Cha wakadiriajiMajenzi Afrika Prof. Robert Pearl akihutubia mkutano wa Wakadiriaji Majenzi uliofanyika kwenye hotel ya Golden Tulip.
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza jambo na Viongozi wa Chama cha Wakadiriaji majengo mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji
Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini
Dar es Salaam.
***********
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka
wakadiriaji majenzi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na
waepuke vitendo vya rushwa katika mchakato wa ukadiriaji majengo nchini.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 18-Aug-16 wakati anafungua mkutano wa mwaka wa wakadiriaji majenzi
kutoka nchini mbalimbali za Afrika jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mchakato wa kuanza
kutekeleza miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa
kiwango cha kisasa (Standard gauge) na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka
nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania na
suala la kuhamia Makao Makuu Dodoma hivyo ni muhimu kwa wakadiriaji majenzi
wakajipanga vizuri katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa kwa kuweka gharama
nafuu kulingana na hali halisi ya mradi unaotakiwa kujengwa.
Amesema
serikali inatambua mchango wa watalaamu wa ukadiriaji majenzi hivyo ni muhimu kwa
wataalamu hao wakauongeza bidii katika utekelezaji wa kazi zao hasa kwa kuzingatia
teknolojia za kisasa.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amehimiza ushirikiano kati wakadiriaji majenzi wa
Tanzania na wa nchi nyingine za Afrika katika kubadilishana uzoefu kwenye kazi
zao ili kuongeza ubunifu na ufanisi katika miradi wanayopata.
Kwa
upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
amesema serikali imetenga dola bilioni 2.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na bandari na
viwanja wa ndege hivyo serikali inahitaji wakadiriaji majenzi waadilifu katika
utekelezaji wa miradi hivyo na sio vinginevyo.
0 comments:
Post a Comment