Meneja wa Bank of Africa (BOA), tawi la Babati, Goodluck Mwasa akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa tawi hilo.
Meneja wa Bank of Africa (BOA), tawi la Babati, Goodluck Mwasa (kulia), akifafanua jambo kwa Kamishna
wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Francis
Massawe. Wa pili kushoto ni mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Longino
Kazimoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa, Ammishaddai Owusu-Amoah akitoa hotuba fupi kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la Babati mkoani Manyara.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Longino Kazimoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa (BOA), Ammishaddai Owusu-Amoah na Meneja wa Tawi jipya la Babati, Goodluck Mwasa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Longino Kazimoto akikata utepe kuashiria
kufunguliwa kwa tawi jipya la Bank of Africa mjini Babati.
Waliokaa kutoka kushoto ni Samson Ntunga, akimuwakilisha Katibu Tawala (Manyara), Mkurugenzi Mtendaji wa wa Bank of Africa, Ammishaddai Owusu-Amoah akiwa na mgeni rasmi, Longino Kazimoto na RPC Franc
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Joel
Bendera, amesema maendeleo ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini
hayawezi kuwa na mafanikio bila ya kuhusisha Sekta binafsi.
Bendera alitoa kauli hiyo, mwishoni mwa wiki katika
sherehe za ufunguzi wa matawi mapya ya benki
ya Tanzania yaliyofunguliwa, Babati mkoani Manyara.
Alisema
Benki hiyo imedhamiria kupanua shughuli za kibenki
nchini hasa katika kukuza uchumi wa watu
wa Babati.
“Benki
hii inakuja na mengi mapya katika
Sekta ya Benki na kuleta huduma za kibenki karibu na wananchi wa Babati ikiungana na Benki zingine pamoja na
kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania,”alisema
.
Bendera na kuongeza “Niombe uongozi pamoja na wafanyakazi wote wa Benki ya Afrika kuhakikisha kwamba wateja wa tawi la Babati wanapata huduma za kipekee katika viwango vya kimataifa tukiweka pamoja na mahitaji ya wana Babati katika benki yenu. natumaini kuwa una wafanyakazi wenye sifa, uwezo na weledi wa kufanya kazi na hivyo unachohitaji sasa ni wateja,”alisema Bendera.
Bendera na kuongeza “Niombe uongozi pamoja na wafanyakazi wote wa Benki ya Afrika kuhakikisha kwamba wateja wa tawi la Babati wanapata huduma za kipekee katika viwango vya kimataifa tukiweka pamoja na mahitaji ya wana Babati katika benki yenu. natumaini kuwa una wafanyakazi wenye sifa, uwezo na weledi wa kufanya kazi na hivyo unachohitaji sasa ni wateja,”alisema Bendera.
Bendera alisema Serikali
inafanya kila iwezalo katika kuhakikisha huduma za kifedha zinamfikia kila
mwanachi kwa urahisi na kwamba katika
kuhakikisha hili linafanyika serikali itaboresha miundombinu hasa barabara,
njia za mawasiliano na utengenezaji wa Sera zilizo stahiki na kupigana na
umasikini.
Aliongeza kuwa Serikali itaendelea na jukumu
lake la kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuhamasisha wawekezaji zaidi
Nchini.
“ Pamoja na jitihada
hizo bado kuna maeneo yanayohitaji kuboreshwa ili kujenga mazingira bora ya
Sekta Binafsi kukua hasa suala la upatikanaji wa huduma za Kibenki Vijijini na
katika Sekta ya Kilimo,”alisema Bendera.
0 comments:
Post a Comment