Nafasi Ya Matangazo

August 02, 2016

Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Rahisi, (Easy Banking), wa BancABC,Thompson Mwasikili, (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha benki hiyo, Joyce Malai,  wakati akizindua huduma mpya ya “Mkoporahisi”, makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Agosti 2, 2016. BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake ambapo mteja wa benki hiyo ambaye ni mtumishi wa serikali anaweza kupatiwa mkopo ndani ya masaa 48
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Rahisi, (Easy Banking), wa BancABC,Thompson Mwasikili, (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha benki hiyo, Joyce Malai.
BANCABC ambayo ni sehemu ya Atlas Mara imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake kwani imeanza kutoa mikopo ndani ya saa 48 kupitia huduma mpya ya ‘mkoporahisi’.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 1, 2016, makao makuu ya benki hiyo, kwenye jingo la Uhuru Hights jijini Dares Salaam, Mkuu wa kitengo cha Easy Banking wa BancABC, Thomson Mwasikili, (pichani juu), alisema wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwavutia wateja wengi zaidi kutoka sekta mbalimbali ikiwemo serekalini ili kuhakikisha wanapata huduma hii kwa haraka.
“Kwa kupitia huduma hii ya mkoporahisi tutahakikisha kuwa wateja wetu ambao ni waajiriwa wa Serikali, wanapata mikopo yao ndani ya saa 48 kuanzia muda ambao maombi yaliwasilishwa..tutalisimamia hili na kuhakikisha linatekelezeka,” alisema Mwasikili. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Bw. Mwasikili alisema benki yake inatoa mikopo ya hadi  Tsh milioni 40 kwa riba ya kiwango cha chini hadi asilimia 1.6 kwa mwezi ambayo ni miongoni mwa riba za chini kabisa katika soko la sasa.
“Waombaji wataweza kulipa mikopo yao kwa muda mrefu wa hadi miaka 6 na hakuna pingamizi kuhusu lini unaweza kuongeza mkopo wako,” alisema na kuongeza kuwa muombaji ana uhuru wa kupata mkopo wa muda mfupi hata wa mwezi mmoja.
Kwa mujibu wa Mwasikili, tofauti na mikopo mingine, waombaji wana uhuru wa kuchagua matumizi ya fedha kwa mfano kulipia ada, kununua gari, kukarabati nyumba, kulipia kodi na kumaliza ujenzi na benki haitamlazimisha mkopaji matumizi ya mkopo wake.
Waombaji pia watapata fursa ya kuchanganya mikopo yao yote na kuwa na mkopo mmoja kwani BancABC inaweza kununua mikopo yote hiyo na kumpunguzia mteja usumbufu.
“Endapo muombaji wa mkopo atafariki, mkopo utafidiwa kupitia bima ya mikopo na fedha kiasi cha Tsh 500,000 taslimu zitatolewa kugharamia mazishi,” alisema.
“Tunatoa rai kwa wateja wetu wote na pia wale ambao hawana akaunti na benki yetu kuchangamkia huduma hii ya mkoporahisi kwani hii ndio benki pekee ambayo inakusogeza karibu na ndoto zako , pata mikopo ndani ya saa 48,” alisema.
Atlas Mara iliorodheshwa katika soko la hisa la London Disemba 2013. Atlas Mara ina lengo la kujitanua na kuwa kinara katika masuala ya kifedha katika ukanda wa sub sahara kwa kutumia uzoefu wake na uwezo wa kukuza mitaji. 

Malengo yake ni kuunganisha na kukuza uwezo wa taasisi za kifedha na pia kuendeleza uchumi katika nchi ambazo inafanya shughuli zake.
Posted by MROKI On Tuesday, August 02, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo