Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto), na Afisa Uhusiano
Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakitazama gari Kaparata kwenye banda la
Shirika la Viwanda Vidogo vidogo SIDO kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Gari
hilo limebuniwa na kutengenezwa na Mtanzania Jacob Luis, wa Kaparata
Engineering.
Mbunifu wa gari hilo, Jacob Luis, akihojiwa na mwandishi wa habari kuhusu ubunifu huo
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MKURUGENZI
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, ametembelea banda la Shirika
la Viwanda Vidogovidogo SIDO kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya
Dar es Salaam, 2016 yanayoendelea pale viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya
Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mayingu
alitembelea banda hilo ili kujionea na kupata maelezo ya kina jinsi shirika
hilo linavyoendeleza viwanda vidogovidogo ambavyo vinahitajika sana kwa sasa
ukizingatia mkakati mkubwa wa serikali ya awamu ya Tano ambayo iemdhamiria kuifanya
bTanzania kwua nchi ya viwanda na hivyo kupanua wigo wa ajira kwa Watanzania.
Mkurugenzi
Mkuu huyo amabye alifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul
Njaidi, alipokelewa na Msimamizi Mkuu wa banda hilo, Kalumuna Benedicto, na
alitembezwa maeneo mbalimbali na kujionea mashine mbalimbali zilizobuniwa na
kutengenezwa na watanzania.
Pia
alipata fursa ya kujionea gari lililobuniwa na kutengenezwa na Mtanzania Jacob
Luis, wa Kaparata Engineering.
Gari
hilo lina injini yenye ukubwa wa CC 900 na linatumia mafuta ya petrol, likitumia
lita moja ya petrol kwa kilomita 15 na linabeba watu watano na mzigo wa kilo
500.
Kwa
mujibu wa maelezo ya mbunifu Jacob Luis, gari hilo ni maalum kwa shughuli za
shamba, kubeba maharusi, shughuli za kijeshi, polisi na zile za kiulinzi.
Mkurugenzi
huyo pia alitembelea mabanda washirika wa PSPF, likiwemo lile linalokusanya
wajasiriamali wanawake kutoka nchi nzima ikiwemo Zanzibar, hali kadhalika
Mkurugenzi Mkuu huyo alitembelea Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Mifuko
ya Hifadhi ya Jamii ya PPF, LAPF, GEPF NA PPF.
Maelezo kuhusu gari Kaparata
Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakati akikagua mashine zilizokuwa zikionyeshwa kwenye banda hilo la SIDO
Muangalizi Mkuu wa banda la SIDO, Kalumuna Benedicto, (kushoto), akimpatia maelezo, Mkurugenzi Mkuu Mayingu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi kuhusu mashine hizi
Muangalizi Mkuu wa banda la SIDO, Kalumuna Benedicto, (kushoto), akimpatia maelezo, Mkurugenzi Mkuu Mayingu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi kuhusu mashine hizi
Mayingu akizungumza jambo mbele ya wafanyakazi wa WCF, wakiongozwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi, Fulgence Sebera, (watatu kulia) wakati akitembelea banda la Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF)
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kushoto), akimpatia maelezo ya kiutendaji ya Mfuko huo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, alipotembelea banda la PPF akifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi
Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akitembelea banda la NSSF
Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akiangalia bidhaa zinazozalishwa na mjasiriamali huyu kutoka mkoani Dodoma
Mkurugenzi Mkuu Mayingu akipata amelezo kutoka kwa mjasiriamali wa mkoa wa Manyara
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF akitembelea banda la LAPF
Mayingu akitembelea banda la wajasiriamali kutoka Kigoma lililoko kwenye jengo la EOTF
Mkurugenzi Muu Mayingu (wapili kulia), akitembelea banda la GEPF kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango
0 comments:
Post a Comment