Wasanii wa Kikundi cha Butterfly Arts Group kilichokuwa
kinafanya maonesho ya sarakasi nchini India, Kulia ni kiongozi wa
kikundi hicho Selemani Pembe, Mwanaidi Abdallah, Abdallah
Mkumba<hamidi Mbwana na Salem Mbugio.
Na
Mwandishi wetu
KIKUNDI
cha sarakasi cha Butterfly Arts Group kimerejea nchini juzi kutoka India
kufanya maonesho ya sanaa ya sarakasi.
Katibu
wa kikundi cha Butterfly Arts Group, Selemani Pembe alisema jana Dar es Salaam
kuwa katika ziara yao ya kikazi nchini India iliyodumu kwa mwaka mmoja ilikuwa
na mafanikio makubwa ambapo wasanii wote sita wa kikundi hicho wamepata mafunzo
ya kutosha ya kufanya maonesho ya sarakasi.
Pembe
ambaye pia ni mwalimu wa Sarakasi nchini aliyewahi kuongoza vikundi vya sanaa
vya DDC Kibisa, Muungano Culture Troup, Makutano Dancing Troup, Ujamaa Ngoma
Troup alisema katika kipindi chote cha kuonesha sanaa ya sarakasi wamegundua
kuna utofauti mkubwa kati ya sanaa za maonesho za Tanzania na India.
Alisema
wacheza sarakasi wa India wanatumia vifaa vya kufunga juu ya jukwaa na kubembea
juu kwa juu tofauti na hapa nchini ambapo hakuna kumbi za kufunga vifaa maalum
kwa ajili ya kuonesha sarakasi hizo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Pembe
alisema pamoja na kasoro hizo sarakasi ya Tanzania imekubalika sana nchini
India hasa staili ya kujenga maumbo (Pyramid, kujenga minara mbalimbali na
kucheza ngoma za asili.
Alisema
maonesho mengine yanayowavutia wanamichezo nchini India ni mchezo wa Limbo
ambao mwanasarakasi anapita katikati ya moto chini ya bomba maalum ambalo
limewashwa moto mkubwa na mchezo mwingine ni ule wa kupanda bomba kwa staili
mbalimbali mithili ya nyani.
Alisema
katika kipindi cha mwaka mmoja walikuwa wakifanya maonesho na Kampuni ya New
Rambo Circus inachofanya maonesho katika miji mbalimbali nchini India na nchi
jirani.
Alisema
wakiwa huko walifanya maonesho katika miji ya Pune, Bangalore, Gujirat, Mumbay
na miji ya mipakani na nchi ya Nepal.
0 comments:
Post a Comment