Balozi wa Kili Challenge ambaye pia ni msanii wa muziki wa kughani, Mrisho Mpoto akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu tukio la kupandisha watu 50 katika kilele cha mlima Kilimanjaro na waendesha baiskeli 50 kuuzunguka mlima huo kwa baiskeli ili kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi. Kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Tenga Tenga. na kushoto ni Kamishina wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Peter Dickson.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Tenga Tenga.(kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu tukio la kupandisha watu 50 katika kilele cha mlima Kilimanjaro na waendesha baiskeli 50 kuuzunguka mlima huo kwa baiskeli ili kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi. katikati ni Balozi wa Kili Challenge ambaye pia ni msanii wa muziki wa kughani, Mrisho Mpoto na kushoto ni Kamishina wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Peter Dickson.
Balozi wa Kili Challenge ambaye pia ni msanii wa muziki wa kughani, Mrisho Mpoto akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu tukio la kupandisha watu 50 katika kilele cha mlima Kilimanjaro na waendesha baiskeli 50 kuuzunguka mlima huo kwa baiskeli ili kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi. Kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Tenga Tenga.
*************
MGODI wa Dhahabu wa Geita, Ukishirikiana na Tume
ya kudhibiti Ukimwi, kwa mwaka wa 15 tangu kuanzishwa kwake, unatarajia
kupandisha watu katika kilele cha Mlima Kilimanjaro watu 50 na kundi lingine
lenye watu 50 watauzunguka mlima kwa baiskeli ili kuchangisha fedha kwaajili ya
mapambano dhidi ya Ukimwi hapa Tanzania.
Tukio hili limnatarajiwa kufanyika Julai 16 hadi
22 mwaka huu na watu kutoka mataifa mbalimbali watashiriki katika tukio hilo la
kihistoria.
“Huu ni mwaka wa 15 tangu kuzishwa kwa Kili
Challenge kwa hivyo tumedhamiria kufanya tukio hili kuwa tukio la kihistoria,”
alisema Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano wa Mgodi wa GGM, Tenga Tenga.
Tukio hili ambalo hufanyika kila
mwakalilizinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais (Muungano na
Mazigira) Januari Makamba kwa niaba ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Kili Challenge katika mwaka huu itakuwa na kundi
kubwa la watu kutoka nchi mbalimbali lakini wengi wakiwa watanzania kutoka katika
sekta binafsi, serikalini, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na watu mbalimbali
waliojitolea ili kutunisha mfuko huu wa Kili Challenge. Balozi wa Kili
Challenge, Mrisho Mpoto ndie ataambatana na kundi hili hadi kileleni.
Balozi wa Kili Challenge, Mrisho Mpoto
alisistiza watanzania kutambua kwamba mapambano dhidi ya Ukimwi ni yetu sisi
watanzania na tunapaswa kuamua kuunga mkono jitihada za serikali kwa ajili ya
kupambana ili kufikia sifuri 3.
“Mimi kama balozi wa Kili Challenge, naamini
kwamba jitihada zinazfanywa na mfuko huu zinahitaji kuungwa mkono na watanzania
wote na wadau wenyemachungu na nchi hii. Hebu tuungane kwa pamoja kila mmoja
wetu katika sehemu yake eidha kwa kuchangia au kumuelimisha mwenzake ili
mapambano haya yalete mabadiliko,”alisema Mpoto.
Mwakilishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania
(tacaids), Dickson Peter alisema Fedha zinazopatikana katika mfuko huu
zinapelekwa kusaidia mapambano dhidi ya ukimwi ikiwa ni pamoja na kujenfa vituo
vya ushauri nasaha na upimaji wa ukimwi ambapo baadhi yao ni vile vilivyopo
mkoani Tanga pale Segera, Manyoni na Geita. Kituo cha watoto yatima Moyo wa Huruma na Asasi nyingine zaidi
ya 30 zimenufaika na mfuko huu.
Tenga alisema GGM inapenda kutambua michango ya
wadau wengine wanaochangia mfuko huu kama vile, ACACIA, Prime fuel, Airtel,
Capital Drilling (T)Ltd na wengineo.
0 comments:
Post a Comment