(Dar es Salaam,
30 Juni 2016) Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa
(TAKUKURU) wamebaini kuwepo na baadhi ya
Makampuni na watu binafsi ambao wamekuwa wakijihusisha na ukwepaji Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya
Mapato kwa kutumia Mashine za Kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na TRA
na kutoa risiti bandia.
Makampuni
hayo yamekuwa yakinunua risiti za manunuzi bandia kutoka kwa watu wanaomiliki
mashine za kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na kuzitumia risiti hizo
kudai marejesho ya VAT bila kuwepo na bidhaa au huduma halisi iliyouzwa au
kutolewa na muhusika, kitendo ambacho kinainyima Serikali mapato stahiki kwa
mujibu wa sheria.
TRA kwa
kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi ili kubaini makampuni yote
yanayojihusisha na udanganyifu huu, ambapo hadi sasa jumla ya makampuni manne (4) yamebainika kujihusisha na ukwepaji kodi kwa mtindo huu
kuanzia mwaka 2010 hadi 2014; na jumla ya shilingi 29,216,900,301.7 imebainika kutokulipwa Serikalini na makampuni
hayo kwa kipindi hicho.
Makampuni hayo
manne ni pamoja na Skol Building Material Ltd ambayo tangu mwaka 2012 hadi 2013 haikulipa jumla ya
VAT ya shilingi 5,464,915,963 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi
10,960,787,861 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 16,425,703,824 kwa
kipindi hicho.
Kampuni
nyingine ni Farm Plant (T) Limited, tangu mwaka 2010 hadi
2014 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 5,930,170,573 na Kodi ya Mapato yenye
thamani ya shilingi 4,948,393,516 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi
10,878,564,089.
Kwa upande
wa A.M. Steel & Iron Mills Limited kuanzia mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya
shilingi 79,016,112 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi 131,693,518 ambayo
jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 210,709,630.
Kampuni
nyingine ni A.M. Trailer Manufacturers Limited ambayo tangu mwaka 2013 hadi
2014 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 638,221,034.80 na Kodi ya Mapato yenye
thamani ya shilingi 1,063,701,724.00 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni
shilingi 1,701,922,758.80
Baada ya kubaini ukwepaji kodi wa makampuni hayo, TRA kwa
kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizi na mara baada ya uchunguzi kukamilika hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kukwepa kodi.
“Ni wito wangu kwa wafanyabiashara wote kutojihusisha
na kununua risiti za bandia na kudai marejesho ya (VAT) yasiyostahili kwakuwa
Mamlaka imejidhatiti kuendelea na zoezi hili la kuwabaini wafanyabiashara wanao
kwepa kodi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa hatua stahiki”. Alisema
Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata.
Imetolewa
na:
Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa
pamoja.
0 comments:
Post a Comment