Wataalamu wa Kilimo kutoka SABmiller Francois Potgieter na Gerhard
Greeff wakikagua mashamba ya wakulima wilayani Karatu walipowatembelea na
kuwapatia ushauri
Wakulima wanapenda kupata ushauri wa kitaalamu ili wapate mafanikio
pichani wakulima wa shahiri wilayani Karatu wakimsikiliza mtaalamu wa kilimo na
mshauri wa TBL Group Dk. Bennie Basson alipowatembelea
Wakulima wanaoshirikiana na TBL wilayani Karatu wakisikiza ushauri wa
wataalamu wa kilimo walipotembelewa hivi karibuni.
****************
Zaidi ya wakulima 700 wa zao la zabibu mkoani Dodoma wananufaika na mpango wa kilimo shirikishi unaoendeshwa na
kampuni ya TDL iliyopo chini ya kampuni ya TBL Group ambao umeanza kuonesha
mafanikio kwa kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji katika mashamba yao ya zabibu.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin amebainisha hayo wakati
akitoa ripoti ya mwelekeo wa biashara ya kampuni W kwa kipindi cha mwaka ujao
ambapo alisema kuwa mpango shirikishi na wakulima wa zabibu umeanza kutekelezwa
katika vijiji vya Bihawana, Mpunguzi, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula, Makang’wa,
Mzakwe na Mbalawala
Alisema kuwa Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa
utaalamu wa kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya Makutupora Viticulture
Training and Research Center (MVTRC) ambapo mafanikio ya mpango huu yameanza
kuleta mafanikio kwa wakulima kupatiwa elimu ya kilimo cha kisasa cha zao la
zabibu na kuanza kufanya utekelezaji kwa kutumia ushauri wa wataalamu wa
kilimo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Katika kuwapatia wakulima motisha wakulima ili wajiunge na waweze kuboresha maisha yao kupitia kilimo
cha zao la zabibu chini ya mpango huu watoto wa wakulima wa zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu
kupitia mfuko
unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza
Jarrin alisema kuwa mpango huu shirikishi tayari umeonyesha mafanikio
makubwa kwa wakulima
wa zao la Shahiri katika mikoa ya kanda ya Kaskazini ambao wengi maisha yao
yamebadilika kuwa bora na kuwepo ongezeko kubwa la ajira kutokana na kilimo cha
zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengeneza kinywaji cha bia.
“Kwa upande wa zao la Shahiri wakulima zaidi ya 3000 wanaendelea
kunufaika.Katika kipindi cha mwaka 2015 mpango huu umewezesha ongezeko la
uzalishaji wa zao hilo kufikia tani 15,574 kiasi ambacho kimevuka lengo la
matumizi na mahitaji ya kampuni”.Alisema.
aliongeza kuwa kampuni
inao mkakati wa kuendelea kufanya kazi na wakulima na kubadilisha maisha yao kupitia mpango wa
kampuni mama ya SABMiller ujulikanao kama Go Farming ambao tayari umeanza kutekelezwa katika nchi mbalimbali
ambazo imewekeza.
Alisema lengo kubwa la mpango huu ni kuinua maisha ya wakulima wadogowadogo,kuongeza
kasi ya kukua uchumi na kujenga mfumo mzuri na endelevu wa kupata malighafi kwa ajili ya viwanda kampuni
ya TBL Group kwa hapa nchini na SABMiller vilivyopo kwenye nchi mbalimbali
barani Afrika
“Mpango wa Go Farming haulengi kunufaisha wakulima wa Shahiri pekee
bali pia wa mazao mengine kama mtama na mihogo na katika siku za usoni wakulima
wa zao la mahindi watawezeshwa pia na inategemewa hadi kufikia mwaka 2020 zaidi
ya wakulima nusu milioni watakuwa wamewezeshwa sehemu mbalimbali duniani ambako
kampuni imewekeza na mamilioni ya wananchi watajipatia riziki kutokana na
kufanya kazi za utekelezaji wake”.
Aliongeza kuwa matarajio ya mafanikio ya mpango huu katika kipindi cha
mwaka 2015 hadi 2020 yanaonyesha kukua kwa asilimia 44 katika nchi 10 ambako
umeanza kutekelezwa na inakadiriwa kuwepo ongezeko la uzalishaji wa mazao
kutoka tani 300,000 kufikia zaidi ya tani 600,000.
0 comments:
Post a Comment