Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma, Dk Jasmini Tiisekwa akizungumza na
wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Dodoma wakati wa uzinduzi wa
programu ya Vsomo inayotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ambapo
wanafunzi wa Chuo cha Veta watapata fursa ya kusoma kupitia simu ya
mkononi
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Dk Jasmini Tiisekwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Dodoma wakati wa uzinduzi wa programu ya Vsomo inayotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ambapo wanafunzi wa Chuo cha Veta watapata fursa ya kusoma kupitia simu ya mkononi
Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Hawa Bayumi, akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Dodoma wakati wa uzinduzi wa programu ya Vsomo inayotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ambapo wanafunzi wa Chuo cha Veta watapata fursa ya kusoma kupitia simu ya mkononi kulia ni Meneja mauzo wa Airtel Dodoma Stephen Akyoo na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Dk Jasmini Tiisekwa
Wanafunzi
wa Chuo cha Veta Dodoma wakimsikiliza Meneja huduma za Airtel Tanzania, Hawa
Bayuni (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango wa Vsomo ambapo wanafunzi
wa Veta watapata fersa ya kusoma kwa kupitia simu ya mkononi.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Dk Jasmini Tiisekwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Dodoma wakati wa uzinduzi wa programu ya Vsomo inayotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ambapo wanafunzi wa Chuo cha Veta watapata fursa ya kusoma kupitia simu ya mkononi
Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Hawa Bayumi, akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Dodoma wakati wa uzinduzi wa programu ya Vsomo inayotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ambapo wanafunzi wa Chuo cha Veta watapata fursa ya kusoma kupitia simu ya mkononi kulia ni Meneja mauzo wa Airtel Dodoma Stephen Akyoo na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Dk Jasmini Tiisekwa
***********
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wakishirikiana na
Airtel kupitia AIRTEL FURSA wamefanya inaendelea kufanya mafunzo ya stadi za
ufundi kuwa katika njia rahisi na nafuu kwa watanzania.
Katika kuhakikisha kwamba vijana wa kitanzania wanafikiwa popote
pale walipo, VETA na Airtel wamewasili katika mkoa wa Dodoma na kutoa fursa ya
mafuzo ya stadi za ufundi katika mkoa huo.
kozi zinazotolewa ni pamoja na ufundi pikipiki, ufundi umeme wa
majumbani, ufundi wa simu za mkononi , ufundi Alluminium, utaalamu wa masuala
ya urembo na ufudi wa kuchomea vyuma.
Kozi zinazotolewa katika awamu hii ya kwanza na VETA kupitia kadi ya
simu ya Airtel zinatolewa kwa bei ya chini kabisa ya Sh.120,000/=.
Muda wa kujisomea kozi ya vitendo katika chuo cha VETA baada ya
kufaulu kozi ya nadharia ni jumla ya masaa 60 . Hii ikimaanisha kuwa mtu
atakayeweka msimamo na kusoma kwa bidii ataweza kumaliza ndani ya mwezi mmoja
na kuweza kupata cheti chake.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Dk Jasmini Tiisekwa alitoa maoni yake juu ya
mafunzo yanayotolewa na VETA kupitia Airtel, alisema, "Nafurahi kwamba
VSOMO imekuwa si tu kwa kuwa bei nafuu lakini pia urahisi wanaoupata vijana
kwani wanaweza kuendelea na shughuli zao za kila siku kama wameajiriwa na
kuboresha ujuzi wao kupitia mtandao pale wanapopata nafasi.
Naona wasichana wengi sasa wataweza kupata ujuzi wa kupika kwa kupitia
simu zao za mkononi.
Akitoa maoni yake juu VSOMO, Mkuu wa chuo cha Veta Kipawa Dar Es
Salaam, Eng. Lucius Luteganya alisema, "Tunaamini mpango wa VSOMO
utabadilisha mtazamo wa vijana wetu na kutumia zaidi teknolojia na kusoma
kupitia mitandao.
Amewahimiza vijana wa Dodoma na mikoa ya karibu kutumia VSOMO kama
fursa ya kuongeza ujuzi ambao unahitajika katika soko hili gumu la ajira.
“Tunafuraha kubwa sana na mpango huu ambao Veta wameweza kuuungana na Airtel
kwa kuweza kubadilisha maisha ya vijana wa kitanzania".
Hii ni wiki ya pili toka kuanzishwa kwa VSOMO ambapo vijana wa Dodoma
walishiriki katika warsha ya kujiunga na VSOMO mwishoni mwa wiki hii, ambapo
vijana wengi walijitokeza na kujiunga na masomo haya ya VSOMO.
VSOMO ni mafunzo ya stadi ya ufundi kwa njia ya mtandao kwa wateja wa Airtel wenye simu za aina ya android, ambapo mteja anatakiwa kupakua VSOMO kwenye orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store na kulipa gharama ya sh 120,000 / = tu.

0 comments:
Post a Comment