Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli akikabidhi tuzo kwa mshindi
wa kwanza wa Tuzo ya Rais ya mzalishaji bora wa mwaka 2015, kwa
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin wakati wa hafla ya
kutoa tuzo kwa washindi iliyofanyika jijini katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam . Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wenye Viwanda
Tanzania (CTI), Dk. Samwel Nyantahe ( wa pili kulia) na kushoto ni Waziri
wa Biashara ,Viwanda na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati
wa hafla hiyo
Rais John Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda
na watendaji wa makampuni ambayo yameshinda tuzo mbalimbali katika kipindi cha
mwaka huu
Mkurugenzi Mkuu wa TBL
Group,Roberto Jarrin (wa nne mstari wa mbele kutoka kushoto) akiwa katika picha
ya pamoja na maafisa wa kampuni hiyo waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa tuzo
************
Kampuni ya TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais
ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa
kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo imetunukiwa tuzo kwa
ushindi huo.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania
(CTI na hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini
Dar es salaam katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni
wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea baada ya hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto
Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni kwa
kuwa jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa
kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona
mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo
mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini na
kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali
za kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda
vyake na mtandao wa wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi
ya kuwasaidia wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa
kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.
“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa karibu na
wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio
zaidi katika siku za usoni”.Alisema.
0 comments:
Post a Comment