MIRADI ya maendeleo yenye thamani ya Sh Bilioni
1.09 inataraji kukaguliwa, kuwekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa na Mwenge wa
Uhuru Wilayani Newala mkoani Mtwara.
Mwenge huo unataraji kukimbizwa Wilayani humo
kuanzia Juni 3 mwaka huu ambapo miradi nane itafikiwa na Mwenge huo utakao
kimbizwa katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza na Habarileo, Mkuu wa Wilaya ya
Newala, Christopher Magala alisema miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha
afya Mkunya, uzinduzi wa Barabara ya lami Newala mjini, kuweka mawe ujenzi wa
nyumba sita za walimu na kufungua kituo cha kilimo Mtangalanga.
“Mwenge wa uhuru utaanza mbio zake Wilayani Newala
kuanzia Juni 3 mwaka huu na utatuzindulia miradi nane ya maendeleo ikiwa ni
pamoja na kituo cha afya, nyumba za walimu, kilimo, na kutembelea vikindi vya
uzalishaji mali vya vijana na wanawake,”alisema Magala.
Magala alisema Mwenge huo pia utapata fursa ya
kutembelea na kujionea vikundi vya uzalishaji mali vya wanawake bana vijana
ambao waliokopeshwa fedha na Halmashauri.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya, alisema kuwa miradi
hiyo nane imegharimu kiasi cha Sh bilioni 1,098629,225 ambapo kati ya hizo
kiasi cha sh milioni 7,850,000 ni mchango wa jamii, huku Halmashauri ikichangia
sh milioni 108,500,000 na serikali kuu ikichangia sh milioni 975,629,225.
Magala aliwaasa wananchi kujitokeza kwa wingi
katika maeneo mbalimbali yatakayokimbizwa Mwenge huo ambao unakimbizwa na
George Mbijima ukibeba kauli mbiu ya ‘Vijana ni Nguvu kazi ya Tifa,
washirikishwe na kuwezeshwa.
0 comments:
Post a Comment