Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema na Meneja Mkuu wa GSM Foundation
Shannon Kiwamba wakiwa kwenye stoo ilipohifadhiwa saruji hiyo.
********
Katika kuhakikisha azma yake ya kuchangia kwa kiasi kikubwa uboreshwaji
wa sekta za elimu na Afya nchini, Taasisi ya GSM Foundation imemkabidhi mifuko
600 ya saruji kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi Sofia Mjema, ambayo itatumika
kuboresha mazingira ya elimu katika Shule ya Msingi Mbande iliyopo kata ya
Chamazi ikiwa ni jitihada za kuboresha elimu kwa kukabiliana na changamoto za
Uwepo wa madarasa uliokuwa unaikabili shule hiyo kwa muda mrefu.
Akiongea katika kukabidhi madawati hayo, Afisa Mawasiliano wa kampuni ya
GSM, Halfan Kiwamba amesema, shehena hiyo ni sehemu tu ya misaada inayotawanywa
nchi nzima na taasisi hiyo yenye lengo la kuwekeza kwenye Afya na elimu bora
kwa kizazi kijacho.
Kiwamba amesema GSM Foundation ina lengo la kusaidia wananchi, hasa wenye
kipato cha chini kuhakikisha kwamba watoto wao wana elimu nzuri na uhakika wa
Afya zao ili waweze kujiandaa vema kulitumikia Taifa la kesho.giza kila chumba
kukaa wanafunzi 45.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema akizungumza na wazazi juu ya
kukabidhiwa, mifuko hiyo 600 ya Saruji katika Shule ya Msingi Mbande leo
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mkuu wa GSM Foundation Shannon Kiwamba.
Sehemu
ya wazazi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema
Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema akiwa kwenye picha ya pamoja na
wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbande mara baada ya kukabidhi mifuko hiyo
600 ya Saruji leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema na Meneja Mkuu wa GSM Foundation
Shannon Kiwamba wakikabidhi mifuko hiyo 600 ya Saruji kwenye uongozi wa
Shule ya Msingi Mbande leo jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment