Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia
sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora akizungumza na ujumbe kutoka
Kampuni ya Oracle Afrika (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake kwa nia
ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia
sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya Oracle Afrika Bw. Cherian Varghese (katikati) akielezea
nia ya Kampuni yao katika ushirikiano wa kulinda miundombinu na mifumo ya
TEHAMA hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Dkt. Mhandisi Maria Sasabo (wa kwanza
kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Oracle Afrika walipotembelea sekta
ya Mawasiliano na kueleza nia yao ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na
mifumo ya TEHAMA.
*****************
KAMPUNi
ya Oracle Sytem Limited kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano itakuwa na mkutano wa The Africa Security Summit
utakaofanyika hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam tarehe 30 Juni,
2016.
Lengo la mkutano huo i kuwakutanisha wadau na wataalamu mbalimbli wa Taasisi za Serikali na sekta binafsi wapatao watu 200 kutoka ndani na nje ya nchi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Bwana Varghese amesema kuwa mkutano huo utawawezesha wataalamu wa watanzania na kuwajengea uwezo na kuongeza uelewa wa usalama wa taarifa na umuhimu wake na namna ya kuzitumia ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa letu. Pia Kampuni yake imetambua na kuona namna ambavyo Tanzania imewekeza na kuthamini Sekta ya Mawasilino kwa kuwa na miundombinu ya kisasa, Sera, sheria na kanuni zinazosimamia Sekta ya Mawasiliano na kutambua mchango wake katika kukuza uchumi.
Prof. Kamuzora aliwaahidi kuwa Wizara itawapatia ushirikiano wa kutosha ili Taifa liweze kunufaika kupitia utaalamu, ujuzi na weledi wa Kampuni ya Oracle ili kuendeleza Sekta ya Mawasiliano nchini
Kampuni hiyo tayari imewekeza na kushirikiana na nchi nyingine za Afrika ikiwemo Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini, Kenya na Uganda kuendeleza Sekta ya Mawasiliano katika maeneoe ya usalama wa taarifa na kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa kutumia njia ya kielektroniki.
0 comments:
Post a Comment