Wafanyakazi wa DarBrew
wakionyesha kinywaji cha Chibuku kwenye chupa ndogo wakati wa kuizindua hivi
karibuni
Kikosi kazi cha
menejimenti na wafanyakazi wa DarBrew wakiwa katika picha ya pamoja
wakati wa kusherehekea kupata tuzo ya SABMiller ya kuendeleza vinywaji vya
asili nchini hivi karibuni.
**********
LICHA ya kuwepo na viwanda mbalimbali vya kutengeneza bia na vinywaji
vingine vya kisasa ikiwemo uingizwaji wa vinywaji hivyo kutoka nje ya nchi
bado idadi kubwa ya watanzania wanatumia pombe za asili na sababu kubwa
inabainishwa kuwa hali hiyo inatokana na vinywaji vya kisasa kuuzwa kwa bei ya
juu.
Utafiti uliofanywa na taasisi ya CanBack kuhusiana na matumizi ya
pombe za asili nchini umebainisha kuwa matumizi ya pombe za asili nchini ni
asilimia 50% ambapo kati ya asilimia hizo vinywaji vya asili
vinavyototengenezwa kisasa viwandani vinatawala kwa asilimia 8% . BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Sababu kubwa ya watumiaji wa vinywaji vya asili ambavyo vingi
vinatengenezwa kwenye mazingira yasiyo salama na vinaendelea kuleta athari
kwenye jamii ni kutokana na bei kubwa ya bia ,wine na vinywaji
vinginevyo vya kisasa ambapo idadi kubwa ya wananchi hawana uwezo wa kumudu
kuvinunua na kuvitumia.
Akitoa ripoti ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha mwaka
2015 na mikakati yake ya mbele katika kipindi cha mwaka 2016/17 kwa waandishi
wa habari hivi karibuni,Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin alisema
kuwa kampuni yake tayari imeanza kutekeleza mkakati wa kuboresha vinywaji
vya asili na kuhakikisha vinaingia katika mfumo rasmi unaotambulika kwa
kuviwezesha kuchangia pato la taifa kwa njia ya kodi ikiwemo kulinda afya za
wananchi.
Jarrin alibainisha kuwa kampuni ya DarBrew imeweza kuleta
mapinduzi ya uuzaji wa pombe za asili nchini kwa kuwawezesha watumiaji kupata
kinywaji cha Chibuku na Nzagamba kikiwa kimefungwa kwa viwango mbalimbali
na katika mazingira ya usafi yanayolinda afya za watumiaji na hivi sasa
imekuja na mkakati wa kuwainua akina mama kimapato kupitia kuuza bidhaa zake
unaojulikana kama Chibuku Mamas ambao hadi kufikia sasa wanawake wapatao 130
wameishajiunga na mpango huu.
Alisema kuwa akina mama wakiendelea kujiunga na mpango huu wataweza
kujikwamua kimapato na kulinda afya zao na wanywaji pia kupunguza uharibifu
wa mazingira kwa kutumia kuni kwa ajili ya kupikia pombe za asili
ambazo zimekuwa zikiuzwa katika vilabu mbalimbali.”Tunawasihi watumiaji wa
vinywaji vya asili kujenga mazoea ya kutumia vinywaji vyenye ubora na
vilivyotengenezwa kwenye mazingira mazuri kwa ajili ya kulinda afya zao”.Alisema
Katika kuhakikisha watumiaji wanamudu vinywaji vya asili vya
Chibuku na Nzagamba alisema kampuni imeanza kusambaza vinywaji hivi
vikiwa kwenye ujazo wa chupa za ukubwa wa aina mbalimbali ili wanywaji wote
waweze kuvipata kulingana na vipato vyao.
Kuhusu mtazamo wake wa hali ya biashara ya kampuni kwa sasa Jarrin
alisema sekta ya uuzaji wa vinywaji inakabiliwa na changamoto mbalimbali
mojawapo ni bei kubwa ya bia ambayo watumiaji wake wengi wanashindwa
kuimudu,kuwepo na vinywaji visivyo katika mfumo rasmi wa ushindani katika
soko,kukosekana kwa motisha katika uzalishaji wa malighafi za kutengeneza
vinywaji nchini kwa kuwa zinatozwa kodi kubwa ya zuio kuliko malighafi
zinazotolewa nje ya nchi.
Alisema baadhi ya mambo yanayostahili kufanyika katika uboreshaji wa
sekta ili iendelee kuchangia pato la taifa ni kupunguza kodi za malighafi
zinazozalishwa nchini kama kimea kinachotumika kutengeneza bia pia kulasimisha
pombe za asili ziende sambamba na vinywaji vya sili vinavyolipiwa kodi na
kuhakikisha vinywaji vya asili vinapatikana katika mazingira ya usafi “Pamoja
na changamoto nyingi zilizopo katika sekta hii tunaendelea kukabiliana nazo na
tumedhihirisha uwezo wetu kwa kuwa na viwanda vyenye ubora wa hali ya juu nchini
Tanzania”Alisema Jarrin
0 comments:
Post a Comment