Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato M. Mssanzya – CP
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiweka vizuri silaha yake aina ya Shortgun mara baada ya
uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais alikuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo hilo la uhakiki wa silaha
***********
TAARIFA YA JESHI
LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu zangu waandishi wa habari,
Leo tarehe 30.6.2016 ndiyo tarehe na siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki
silaha. Kwa mujibu wa takwimu za silaha tulizonazo inaonyesha kwamba wapo
baadhi ya wamiliki wa silaha ambao hawajatekeleza agizo la kuhakiki silaha
wanazozimiliki.
Kufutia hali hiyo, natoa angalizo kwa wale wote ambao hawajahikiki silaha
zao kwamba muda wowote kuanzia sasa tutaanza operesheni maalum ya kutafuta silaha
ambazo hazijahikikiwa. Ifahamike kwamba
yeyote atakaye kutwa na silaha ambayo haijahakikiwa atachuliwa hatua kali za
kisheria ikiwemo kupoteza sifa ya kuwa
mmiliki halali wa silaha hiyo.
Tunatoa agizo kwa wamiliki binafsi wa maghala ya silaha waziwasilishe
silaha hizo pamoja na nyaraka zake katika vituo vya karibu vya Polisi kwa ajili
ya uhakiki.
Imetolewa:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi
0 comments:
Post a Comment