Meya wa Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, Charles Kuyeko akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Mtakuja Kata ya vingunguti baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama katika kata hiyo leo.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, Charles Kuyeko (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika Kata ya vingunguti alipokwenda kuzindua mradi wa maji na vyoo katika Kata hiyo leo. Pamojane ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto.
MEYA
wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko amezindua mradi wa maji na vyoo viwili vya
kulipa katika Kata ya Vingunguti Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam leo.
Uzinduzi
wa miradi hiyo ni jitihada za Manispaa Katika kuonyesha dhamira ya kutatua kero
sugu za wananchi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo na viunga vyake.
Miradi
hiyo miwili iliyojengwa katika Kata ya Vingunguti, mtaa wa Mtakuja na mtaa wa
Mtambani imejengwa na CIUP chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.
Awali
akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mtakuja, Sharifu Abdallah Mbulu alisema kuwa miradi
hiyo ilikuwa ijengwe na kukamiliki toka mwaka 2013 lakini kutokana ubadhirifu
na usimamizi mbovu wa uongozi uliopita walishindwa kusimamia ujenzi wa miradi
hiyo na kukamilika kwa wakati. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Uongozi mpya wa mtaa wa mtakuja uliongia mwaka
2014 kwa kushirikiana na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani
wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto kwa muda mfupi wamefanikiwa
kuikamilisha miradi hiyo.
Naibu
Meya na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto akizungumza katika uzinduzi huo
alisema mradi huo utakuwa na faida tatu ambapo mradi wa Maji umelenga kuwaondolea wananchi wa
mitaa adha ya Maji, kuboresha usafi wa mazingira kwani wananchi hasa
wafanyabiashara walikuwa wanakojoa hadharani na kuelekea kuchafua mazingira na
mapato ambayo yatapatikana kutokana na watu kulipa fedha.
Kumbilamoto
alitumia nafasi hiyo kupiga marufuku uchafuzi wa mazingira hasa kukojoa hovyo
kwani sasa hakuna kisingizio tena.
Alimweleza
Mstahiki Meya wa Ilala kuwa Kata ya Vingunguti pia inakabiliwa na changamoto ya
baadhi ya mitaa kutokuwa na maafisa watendaji. Kata inamitaa Sita lakini mitaa
mitatu ndiyo ina maafisa watendaji na mitaa mitatu haina watendaji hali ambayo
inarudisha nyuma utendaji kazi. Lakini changamoto nyingine ni kufufua visima
vya Maji katika mitaa minne iliyobakia ya Kata hiyo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi
huo , Charles Kuyeko akizungumza katika uzinduzi huo amempongeza Diwani wa Kata
ya Vingunguti na viongozi wenzake wa mitaa yote ya Kata hiyo.
Kuyeko
amewapongeza pia wananchi wa Kata ya Vingunguti kwa kuchagua viongozi
wachapakazi na wenye shauku ya kuwaletea maendeleo wananchi wao na kusemafaida
ya kutumia vizuri haki ya kupiga kura ni kuchagua kiongozi bora ambaye ni
mwakilishi wa wananchi na mwenye uwezo wa kutatua kero za wananchi wake ambapo
Vingunguti mmefanikiwa.
“Vingunguti
ninaijua vizuri sana, lakini Vingunguti ninayoijua siku zote siyo hii ya leo,
imebadilika sana imekuwa safi na hata nyuso za watu wake zimebadilika,
zinaonyesha matumaini mazuri tofauti na zamani,” alisema Kuyeko.
Aidha, Kuyeko aliwataka wananchi wa Kata ya
Vingunguti bila kujali itikadi zao watoe ushirikiano wa dhati kwa Diwani kwani
nimchapakazi na mpenda maendeleo.
“Diwani
wenu ni Naibu Meya wa Ilala hivyo kiitifaki ni msaidizi wangu mkuu kwa nafasi
hiyo nimepata fursa ya kumfamu vizuri ni mchapakazi, mpenda maendeleo kwa hiyo
mkimpa ushirikiano mzuri maendeleo mnayoyataka mtayapata,” alisema Kuyeko.
Meya
pia ametumia nafasi kuwataka Madiwani wote wa Ilala kuiga mfano wa Diwani wa
Vingunguti kuwa karibu na wananchi wao ili kujua changamoto zinazowakabili. Kuyeko
amewataka Madiwani kushirikiana na wananchi wa Kata zao kubuni miradi
mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wao.
“Wapiga
kura wanamatumaini na sisi, maana wakati tunaomba kura tuliahidi Mabadiliko,
Mabadiliko hayo ni kuleta maendeleo kwa wananchi wetu,” alisema Kuyeko.
Kuyeko
pia alisema kwa nafasi yake ya kuwa Meya wa Ilala kwa kushirikiana na Madiwani
wote miradi ya maendeleo itafanikiwa.
Mstahiki
Meya amechangia Tshs. 5,000,000/ ili zisaidie kusukuma miradi ya maendeleo kwa
Kata ya Vingunguti hasa kufufua visima vya Maji kwa mitaa iliyobakia.
Uzinduo
huo ulihudhuriwa na wananchi pamoja na viongozi wa Ukawa Kata ya Vingunguti.
0 comments:
Post a Comment