Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akikagua mzigo wa John Evarist ambaye
ni mfanyabiashara aliyekua akipita
kutoka nchini Kenya kupitia mpaka uliopo
katika kijiji cha Kamkunji, mkoani
Kilimanjaro. Katibu Mkuu yuko mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa
na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia
nchini.
Mfanyabiashara John Evarist aliyekua akipita
kutoka nchini Kenya kupitia mpaka uliopo
katika kijiji cha Kamkunji, mkoani
Kilimanjaro, akijibu maswali aliyoulizwa na Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili,
ACI Kagimbo Hosea(wa kwanza kushoto).Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira aliyepo mkoani Kilimanjaro
katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa
na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo
Hosea ( aliyenyoosha mkono), akimuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), mwisho wa mpaka
unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kukagua
njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.Wa pili kushoto ni Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, RPC Wilbrod Mutafungwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akipanda Mlima kwenda kukagua jiwe linalotenganisha nchi ya
Tanzania na Kenya katika Mpaka uliopo eneo la Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu
Mkuu yupo mkoani Kilimanjaro katika
ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na
wahamiaji haramu kuingia nchini.
Ujumbe ulioongozana na Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(), ukishuka kutoka
mlimani baada ya ukaguzi wa mpaka
uliopo Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi
ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu
kuingia nchini.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO
SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
0 comments:
Post a Comment