Benki ya NMB PLC imeanza kutoa hati fungani ya NMB yenye riba ya 13% kwa yeyote mwenye nia ya kuwekeza na kupata faida nzuri. Hii ni mara ya kwanza kwa NMB kutoa hati fungani ya namna hii na inaweza kununuliwa kupitia matawi yote ya NMB au kwa mawakala wanaotambulika kwa kiasi cha chini cha shilingi 500,000 (laki tano tu). Kufunguliwa kwa hati fungani ya NMB kwa wananchi ni matokeo ya kupata kibali kutoka mamlaka ya masoko ya mitaji nchini - Capital Markets & Securities Authority (CMSA).
Wawekezaki wa hati fungani ya NMB watapata riba ya asilimia 13 kwa mwaka itakayolipwa kila baada ya miezi sita kwa miaka mitatu mpaka mwezi Juni 2019; Riba itakayotolewa itakatwa kodi ya mapato. Hati fungani ya NMB inauzika pia, na mteja anaweza kuiuza kwa mnunuaji mwingine na kupata fedha yake kabla ya kmukomaa kwa hati fungani – yaani miaka mitatu. Wawekezaji wanaweza kuiuza hati fungani hiyo kabla ya kukomaa katika soko la wazi kupitia mawakala wa soko la mitaji – kwa kufuata misingi ya soko la hisa la Dar es Salaam.
Hati fungani ya NMB itauzwa kuanzia tarehe 10 Mei, 2016 mpaka June 8 2016 na riba itaanza kulimbikizwa kuanzia tarehe hii. Kununua hati fungani ya NMB, mteja anatakiwa kutembelea tawi lolote la NMB kati ya matawi 175 nchini kote au kwa mawakala wanaotambuliwa.
Tembelea tawi na NMB kunua hati fungani hii na hakikisha umebeba viambatanishi vifuatavyo;
- Fomu ya bondi iliyokamilika na kusainiwa
- Nakala ya kitambulisho
- Akaunti ya CDS
- Kianzio cha fedha cha shilingi 500,000
- Taarifa za akaunti yako ya benki.
0 comments:
Post a Comment