JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTEUZI
WA WENYEVITI NA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA MAKUMBUSHO YA
TAIFA, TAASISI YA UTAFITI WA MISITU TANZANIA (TAFORI) NA BODI YA UTALII TANZANIA
(TTB).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Shirika la Makumbusho ya Taifa, Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu
Tanzania (TAFORI) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Katika uteuzi huo Mhe. Rais amemteua Bi. Anna Abdallah (Mbunge Mstaafu) kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la
Makumbusho ya Taifa, Dkt. Felician
Kilahama (Mbobezi katika fani ya Misitu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)
na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB). BOFYA HAPA KUONA WAJUMBE WA BODI HIZO.
Kufuatia uteuzi huo wa Mhe. Rais, Waziri
wa Maliasili na Utalii kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Shirika la Makumbusho ya Taifa Sura ya 281 kifungu cha 4(2) kikisomwa pamoja na Jedwali aya ya (1a) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi hiyo;
1. Dkt. Amina Amer Issa, Mkurugenzi wa Makumbusho,
Nyaraka na Mambo ya Kale
Zanzibar.
2. Dkt. Ali
S. Mcharazo, Mkurugenzi wa Tanzania Library Services, Dar es Salaam.
3. Prof.
Godius Kahyala, Dean, College of Arts and Social Sciences, University of Dar es
Salaam.
4. Prof.
Thomas J. Lyimo, Dean, Faculty of Science University of Dar es Salaam.
5. Dkt.
Oswald Masebo, Mhadhiri, Mkuu wa Idara ya Historia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
6. Bw.
Lota Melamari, Consult, Management of Natural Resources and Environment and Coordinator of Tanga
Botanical Gardens, Arusha.
7. Dkt. Anna
M. Kishe, Mtaalam wa lugha za Kiswahili na Kiingereza na Mhadhiri katika Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania, Dar es Salaam.
8. Bw.
Donatius M. Kamamba, Mkurugenzi wa Mambo ya Kale, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Aidha, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria
ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania
(TAFORI) Sura ya 277 kifungu cha
6(2) kikisomwa pamoja na Jedwali la 2 (1)(a),
Mhe. Waziri amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi
hiyo;
1.
Prof. Salim Maliondo, Profesa wa Biologia
ya Misitu Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
2.
Dkt.
Susana Augustino, Mhadhiri Mwandamizi matumizi ya mazao ya misitu, Chuo Kikuu
cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
3. Bw. Deusdedit Bwoyo, Kaimu Mkuruenzi
Msaidizi, Maendeleo ya Misitu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es Salaam.
4. Prof. Dismas L. Mwaseba, Director of SUA
Centre for Sustainable Rural Development (SCSRD), Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine, Morogoro.
5.
Bw.
Charles Maguta Kajege, Business Consulatant (Finance), Dar es Salaam.
6.
Dkt.
Lemayon Melyoki Mkurugenzi, Shule ya Ujasiriamali, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
7.
Dkt.
Tuli S. Msuya, Katibu Tawala, Mfuko wa Misitu Tanzania, Wizara ya Maliasili na
Utalii, Dar es Salaam.
8.
Dkt. Emma Liwenga, Mtafiti Mwandamizi,
Taasisi ya Tathmini ya Maliasili (IRA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
9.
Dkt.
Lawrence Mbwambo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania
(TAFORI), Morogoro.
Pia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria
ya Bodi ya Utalii Tanzania Sura ya 364 kifungu cha 3(2) kikisomwa pamoja na Jedwali 1(2), Mhe. Waziri amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi wa taasisi hiyo;
1.
Bw. Ibrahim Mussa, Mkurugenzi wa Masoko,
TANAPA
2.
Balozi
Joseph Sokoine Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki
Kikanda na Kimataifa.
3. Bw. Mark Leveri, Mtaalam wa kutengeneza filamu
na matangazo ya video, Ex. Tanzania Film Company.
4. Bw. Richard Rugimbana, Mtendaji Mkuu Tanzania
Confederation of Tourism (TCT).
5. Bibi.
Zabein Muhaji Mhita, Mbunge Mstaafu na Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi Mstaafu.
6. Agustine
Kungu H. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera na Uchumi, Wizara ya Fedha na Mipango.
Uteuzi wa Wenyeviti na Wajumbe hao ni wa
muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe 24/04/2016 hadi tarehe 23/04/2019.
IMETOLEWA
NA:
Angelina E.A.
Madete
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA
YA MALIASILI NA UTALII
10
Mei, 2016
0 comments:
Post a Comment