Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Eng.
Joseph Nyamhanga
SERIKALI
kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imetangaza rasmi tozo
zitakazotumika katika Daraja la Nyerere jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
(Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, amesema kuwa tozo hizo zitaanza
kutumika rasmi Jumamosi wiki hii na zitahusisha vyombo vyote vya usafiri.
“Hakikisheni
mnazifahamu tozo zote zitazotumika katika daraja hili kwa magari ya aina zote
ili kuondoa usumbufu wakati wa utekelezaji wa zoezi la malipo”, Amesema Eng.
Nyamhanga.
Katibu
Mkuu huyo amezitaja tozo hizo kuwa ni pikipiki zitatozwa shilingi 600,
mikoteteni, Guta, Bajaji, na magari madogo yatatozwa shilingi 1500, wakati
magari aina ya ‘pick up’ yatakayozidi tani mbili na mashangingi yatatozwa
shilingi 2000.
Amefafanua
kuwa mabasi yanayobeba abiria wasiozidi 15(mini bus) yatatozwa shilingi 3000,
mabasi yanayobeba abiria kuanzia 15 hadi 29 yatatozwa shilingi 5000. Mabasi
yanayobeba abiria zaidi ya 29, Trekta na magari makubwa yenye uzito wa tani 2-7
yatatozwa shilingi 7000.
Ameongeza
kuwa matrekta yenye matrela, magari makubwa yenye uzito wa tani saba hadi 15
yatatozwa shilingi 10,000 wakati magari yenye uzito wa tani 15 hadi 20 yatatozwa
shilingi 15,000.
Katibu
Mkuu Nyamhanga ameongeza kuwa magari yenye uzito usio wa kawaida (abnormal
load) yatapita kwa vibali maalum vinavyotolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano na kusisitiza kuwa tozo zote zimezingatia maoni ya wadau na hali ya
uchumi wa wananchi ili kumudu gharama za matumizi ya daraja hilo.
“Magari
yote ya Serikali na taasisi za umma yatatakiwa kulipa tozo kama ilivyobainishwa
isipokuwa yale yenye namba za jeshi (Magereza, Polisi, JWTZ, Zimamoto) na
magari ya wagonjwa”, amesisitiza Eng. Nyamhanga.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Uwekezaji kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (N.S.S.F), Yacoub
Kidula, amewataka wananchi kuchangia gharama za uendeshaji wa daraja hilo ili
kuongeza mapato ya Serikali.
Takribani
wiki tatu magari yamekuwa yakivuka katika Daraja la Nyerere bila tozo ambalo
lilifunguliwa katikati ya mwezi Aprili mwaka huu na Rais wa awamu ya Tano Mhe.
John Pombe Magufuli.
0 comments:
Post a Comment