Konstebo
Said Sengendu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kituo cha Ilala akitoa
maelezo ya utumiaji wa vifaa mbalimbali vilivyopo katika magari ya
kuzima moto na maokozi kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias
Andengenye . (Picha na FC Godfrey Peter)
***********
Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali alipata fursa ya kukagua mradi wa ujenzi wa bwalo la chakula liliopo mkoa wa kinondoni kwa ajili ya kurahisisha upatikani wa huduma kwa askari.
Pia amesisitiza kufufua visima vya maji ya kuzima moto (fire hydrant) kwa kushirikiana na ofisi ya idara ya maji ili kurahisisha kupatikana kwa maji yanapohitajika na jeshi la zimamoto na uokoaji.
Amesema kuwa kwa kushirikiana nao itasaidia kufufua visima vilivyokufa au kuingiliwa na makazi ya wananchi na kufanya zoezi la upatikanaji wa maji ya kuzima moto kuwa karibu na wazimamoto watapata maji na kurudi kwenye tukio kwa haraka zaidi.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (wa kwanza
kushoto) akiongozwa na Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu
Msaidi Peter Mabusi wakikagua mradi wa ujenzi wa bwalo la chakula
lililopo katika kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Lugalo.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (aliyeketi
kulia) akipokea taarifa ya utendaji kazi kutoka kwa Kamanda Kanda
Maalumu ya Dar es salaam, Kamishna Msaidi, Jesuald Ikonko alipotembelea
kituoni hapa leo hii mapema asubuhi katika ziara ya kutembelea vituo
vya zimamoto nchini.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akipokea
maelezo kutoka chumba cha mawasiliano namna ya upokeaji taarifa ya
miito ya dharura .
0 comments:
Post a Comment