Mwanaharakati kutoka mtandao
wa kijinsia Tanzania (TGNP), Bi Gema Akilimali akizungumza na waandishi wa
habari wakati akitoa shukrani fupi kwa uongozi wa DAWASCO kutokana na jitihada
zilizofanyika katika kuboresha huduma ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es
salaam hususani maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini. Kushoto ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja.
************
WANAHARAKATI WA Mtandao wa
kijinsia (TGNP) wamepongeza juhudi zinazofanywa na Shirika la Majisafi na Majitaka
Dar es salaam (Dawasco), kutokana na Mabadiliko na jitihada zinazofanywa na
Dawasco za kuboresha huduma ya Maji pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii
inayoizunguka.
Akizungumza katika kikao cha
pamoja na Dawasco, Mratibu wa kampeni ya Maji ya “MAMA TUA NDOO KICHWANI”
kutoka Mtandao wa Kijinsia Bi. Martha Samwel. Ameitaka Dawasco kuhakikisha
inapeleka huduma ya Majisafi na salama katika sehemu zote muhimu ikiwamo
mashuleni na hospitalini ili kumpunguzia mwanamke adha ya kutafuta Maji kutoka
umbali mrefu pamoja na kumuondolea mwanamke adha ya kubakwa na hata kupigwa
kutokana na kuhangaika kutafuta Maji.
“Tunataka kutoa salamu za
pongezi kwa DAWASCO kwa mabadiliko na
jitihada tunazoziona za kuboresha huduma ya Maji na kufanya kazi ya
kusaidia jamii, tumefurahishwa na jitihada zenu, tutafanya kazi pamoja ili kuhakikisha
tunamuondolea mwanamke shida ya kupoteza muda mwingi kuhangaika kutafuta Maji kwani kampeni yenu ya “MAMA TUA NDOO YA MAJI
KICHWANI” ndio kampeni yetu” alisema Bi. Martha.
Aidha, Mwanaharakati wa
mtandao wa kijinsia Bi. Gema Akilimali, amefurahishwa ya kampeni ya Mama tua
ndoo kichwani kwani itamsaidia mwanamke kwa kiasi kikubwa kushiriki kikamilifu
katika kujenga uchumi wa nchi, kitendo ambacho kwa sasa hatimizi ipasavyo
kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta maji, pia anaamini utaongeza ufaulu
mashuleni kwani badala ya watoto wa kike kutumia muda mwingi kutafuta Maji sasa
wataweza kuokoa muda na kuwa kushiriki masomo ipasavyo.
“Wanawake wanatumia muda mwingi kutafuta Maji,
hivi ni saa ngapi ataleta maendeleo ya nchi? Lazima tumkwamue mama katika janga
hili ili na yeye aweze kujenga nchi yake” alisema Bi. Akilimali.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji
mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amehaidi hadi kufikia Disemba 31
watahakikisha kampeni ya mama tua ndoo ya Maji kichwani itawafikia wakazi wengi
wa Dar hususani wale walio katika tabaka la chini.
Aidha amehaidi kutoa huduma
ya Majisafi na salama bure kwa wazee, walemavu na yatima wote ambao hawana
uwezo wa kumudu gharama za kuunganisha huduma ya Maji, pamoja na kujenga pointi
za ya kunywea Maji katika sehemu mbalimbali za Jiji ikiwa ni pamoja na maeneo
ya stendi ya Mabasi ya Ubungo, Buguruni
chama, Magomeni Mapipa na Kisutu stendi ya zamani.
“Mimi pamoja na menejimenti
yangu tunaenda kumtua mama ndoo ya Maji kichwani mpaka kufikia mwishoni wa mwaka
huu, kwani Maji yatakuwa mengi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es
salaam pamoja na Pwani” alimalizia Mhandisi Luhemeja
0 comments:
Post a Comment