Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo
cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai akitoa mada kwa wafanyakaziwa
kampuni ya TBL jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya masuala ya usalama
wakati kuadhimisha Siku ya Afya na Usalama Duniani.Semina hiyo ilifanyika
kiwanda cha TBL cha Ilala.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL
wakisikiliza mada wakati wa semina ya usalama kazini wakati wa maadhimisho ya
siku ya Afya na Usalama Duniani
Mmoja wa wafanyakazi wa TBL akiuliza swali wakati
wa semina ya usalama kazini wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama
Duniani iliyofanyika kiwanda cha ilala jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa masuala ya afya na jamii Lilian
Msaki,akitoa elimu kwa wafanyakazi wa TBL wakati wa semina ya usalama kazini
wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama Duniani iliyofanyika kiwanda
cha ilala jijini Dar es Salaam. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Maofisa wa Jeshi la Polisi na TBL
wakibadilisha mawazo muda mfupi baada ya kumalizika kwa semina semina ya
usalama kazini wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama Duniani
iliyofanyika kiwanda cha ilala jijini Dar es Salaam.
*************************
Wafanyakazi wa
kampuni ya TBL Group na wanajamii wote wameaswa kuzingatia kanuni za usalama na
kuzitekeleza wakati wote ili kuepuka uwezekano wa kupata majanga ambayo
yanaweza kuepukika .
Wito huo
umetolewa na Meneja anayesimamia mazingira ya sehemu za kazi na Usalama
wa kiwanda cha TBL Group ,Renatus Nyanda wakati akihojiwa kuhusiana na
maadhimisho ya Siku ya Usalama Kazini Duniani ambayo imeadhimishwa na kampuni
hiyo kwa kushirikisha wafanyakazi wake wote .
Nyanda alisema
kuwa linapozungumziwa suala la usalama mahali pa kazi wengi wamekuwa wakidhani
kuwa unapaswa kuzingatia kanuni za usalama unapokuwa kazini tu,dhana ambayo alidai
kuwa ni potofu kwa kuwa Usalama unapaswa kuzingatia wakati wote na mahali
popote na kuwa suala la usalama linamhusu kila mtu awe mfanyakazi waofisini,kiwandani, mkulima, mfanyabiashara na shughuli nyinginezo.
Alisema kampuni
ya TBL Group imekuwa ikilipa kipaumbele suala la usalama kwa wafanyakazi wake
ambapo tayari imefanikiwa kupunguza matukio ya ajali kazini kwa
wafanyakazi wake kutokana na utekelezaji wa mpango wa tahadhari za kiafya na
usalama wa kampuni mama ya SABMiller ambao umefanyiwa utafiti wa kina na wenye
kutoa maelekezo ya kuepusha ajali sehemu kazini na maeneo mengine mbali na
kazini.
Alisema elimu
hii ya tahadhari na usalama ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na
kutekelezwa kwa vitendo haiwasaidii wafanyakazi wanapokuwa kazini tu bali hata
wawapo majumbani kwao au sehemu yoyote nyingine wakiitumia itawasaidia
kuwaepusha na majanga mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza katika shughuli
za maisha ya kila siku.
“Programu hii
inayojulikana kama Safety around Bevarage inafundisha masuala mengi
kuhusiana na usalama kazini ambapo tangu ianze kutekelezwa na kampuni ya TBL
Group imeanza kuonyesha mafanikio katika ofisi na viwanda vyake vyote kwa
kuwa ni nadra matukio ya ajali kujitokeza kwa wafanyakazi na wageni
wanaotembelea kampuni na taasisi nyingi zinavutiwa kuja kwenye kampuni yetu
kujifunza masuala ya usalama”.Alisema
Katika
kuadhimisha siku hii wafanyakazi walishiriki semina zinazohusiana na masuala ya
usalama zilizotolewa na serikali kupitia jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani pia wataalamu wa masuala ya bima na Afya ya jamii walitoa mada
kuhusiana na umuhimu wa kuwa na bima.
Maadhimisho ya
siku ya Usalama kazini Duniani huadhimishwa Aprili 28 kila mwaka ambapo
kampeni za kuhamasisha usalama mahali pa kazi hufanywa na taasisi mbalimbali
duniani kote.
0 comments:
Post a Comment