Kaimu Mkurugenzi wa USAID Tanzania Daniel
Moore ,akiwahutubia wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki kwenye
matembezi hayo.
*************
Wafanyakazi
wa TBL Group mwishoni mwa wiki walishiriki katika matembezi ya siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika jijini Dar e salaam na
kushirikisha serikali, makampuni , mashirika mbalimbali ya serikali na yasio ya
kiserikali na wadau wengine wa sekta ya afya.
Matembezi
hayo ya kilometa tano yalianzia katika viwanja vya Green vilivyopo
Oysterbay na kumalizikia katika uwanja huo TBL ni miongoni mwa makampuni ambayo yana lengo la
kuziwezesha sekta binafsi kuhimiza kuzuia na kutoa huduma za matibabu za
Malaria na kuwa na maono ya kuitokomeza kabisa.
Mratibu
wa mpango wa Afya Bora
wa TBL Group,Julieth Mgani amesema kuwa wameshiriki matembezi hayo Malaria ni
moja ya vipaumbele vilivyopo kwenye mpango wa kampuni na dhamira kuu na maono ya kampuni ni kutokuwa na maambukizi ya
Malaria kabisa ifikapo mwaka 2020.
Wafanyakazi wa Kampuni ya TBL Group wakijiandikisha kushiriki katika matembezi ya kuadhimisha siku ya Malaria.
Wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali
walioshiriki kwenye matembezi ya Siku ya Malaria
wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa USAID Tanzania Daniel Moore wakati
wa matembezi ya Siku ya Malaria
. Baadhi ya washiriki wa matembezi ya Kilomita Tano, wakigawiwa
Kinywaji cha Grand Malt.
0 comments:
Post a Comment