Nafasi Ya Matangazo

April 13, 2016

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Wabunge wa bunge la Arika Mashariki, (EALA), kutokaTanzania, wameendelea na ziara yao ya kutembelea vyombovya habari hapa nchini, ikiwa ni mkakati wa Jumuiya hiyo, kushirikisha vyombo vya habari ili kuwafahamishawananchi wa nchi hizo manufaa ya jumuiya hiyo kwao. 

LeoAprili 13, 2016, wabunge hao wakiongiozwa na Mwenyekiti wao Mh. Makongoro Nyerere, wametembelea kampuni ya The Guardian, wachapishaji wa magazeti ya The Guardian, Nipashe na Lete Raha, na kupata fursa ya kuelezwa shughuli zifanywazo na waandishi wa habarikwenye kampuni hiyo ambapo walitembelea kitengo cha habari mtandao, (E-NEWS), kitengo cha usanifu gazeti na kumalizia kwa mkutano wa kubadilishana mawazobaina ya wabunge hao na uongozi wa chumba cha habari cha The Guardian. 

Pichani, msanifu wa gazeti la The Guardian, Ben Mgana (aliyekaa), akiwaonyesha jinsi gazeti hilo linavyoandaliwa kabla ya kuchapishwa. Wakwanza kushoto ni Mhari Mtendaji wa gazeti hilo, Wallace Maugo, Mkuu wa chumba cha Habari cha The Guardian, Jesse Kwayu, (wapili kushoto) na wabunge wa hilo wakiongozwa na wmenyekiti wao Mh. Makongoro Nyerere (watatu kulia)
 MhaririMtendaji wa The Guardian, Wallace Mauggo, (watatu kushoto) na Mhariri Mkuu wa Chumba cha Habari cha The Guardian Limited, Bw. Jesse Kwayu) wakiwaonyesha wabunge hao baadhi ya magazeti yanayochapishwa na kampuni hiyo
 Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, 9wapili kulia), akisalimianana Mkuu wa kitengo cha habari mtandao (E-NEWS), cha The Guardian Limited, Mashaka Mgeta, wakati wabunge hao walipotembelea chumba cha Habari cha The Guardian Mikocheni jijini Dar es Salaam. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
 Mashaka(kushoto) akisalimiana na Mbunge Mh. Nderakindo Kessy
 Mauggo (kushoto), akitoa maelezo kwa wabunge hao
"Sisi The Guardian, tukotayari kushirikiana na wabunge wa EALA, katika kuujulisha umma kuhusu manufaa ya jumuiya na nitoe wito kwa mbunge mmoja mmoja au kwa kupitia kundi lenu, mpatabo jambo muhimu mnalotaka jamii ilifahamu msisite kutujulisha nasi tutashirikiana nanyi" Jesse Kwayu (kushoto). Anayemsikiliza ni Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere.
"Tuko tayari kuweka column maalum kwa ajili ya shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki, miongoni mwenu mnaweza kuchangia kwa kuandika" Wallace Mauggo 
 "Lazima tukienzi Kiswahili ninampongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuonyesha njia" Mh. Nderaikindo Kessy
 "Waambieni Watanzania waondokane na uoga ni wakati muafaka sasa kwa wananchi wa Jumiya ya Afrika Mashariki kushiriki katika fursa za kiuchumi katika mfumo wa soko la pamoja, ili wmananchi wa Kigoma aweze kuvuka mpaka na kuingia Bunjumbura kuuza mihogo yake" Mh. Makongoro Nyerere
 "Tunaomba ushirikiano zaidi wa vyombo vya habari katika kutangaza fursa za kiuchumi zilizoko kwenye Jumuiya lakini pia ninaomba tuungane pamoja katika kuhakikisha Kiswahili inakuwa lugha rasmi ndani ya bunge la Afrika Mashariki." Shy-Rose Bhanji
 Jesse akisikiliza kwa makini
 Mh. Bernard Murunya (kulia), akimuonyesha kitu Mashaka Mgeta
 Picha ya pamoja, kutoka kushoto), Mh. Nderaikindo Kessy (Mb), Mh. Bernard Murunya (Mb.), Bw. Wallace Mauggo (Mhariri Mtendaji The Guardian), Mh Twaha Taslima (Mb), Bw. Jesse Kwayu, (Mkuu wa chumba cha Habari The Guardian Ltd), Mh. Makongoro Nyerere (Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania), Mh.Maryam Mohammed (Mb),Mh. Shy-Rose Bhanji (Mb) na Bw.Asheri Michael
 Jesse (kushoto), Mh. Makongoro Nyerere, na Bw. Wallace Mauggo
 Mh. Nderaikindo Kessy
 Mh. Bernard Murunya (kushoto) na Mh. Maryam Mohammed
 Mh. Maryam Mohammed
 Mh. Twaha Mussa Taslima, (kushoto) na Mh. Shy-Rose Bhanji
Wabunge kutoka kulia, Mh. Shy-Rose Bhanji, Mh. Twaha Mussa Taslima, Mh. Makongoro Nyerere, Mh. Maryam Mohammed, Bw.Asheri Michael wakimsikiliza MhaririMkuu wa chumba cha Habari cha The Guardian Limited, Bw. Jesse Kwayu
Posted by MROKI On Wednesday, April 13, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo