Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella, akitoa
hotuba rasmi wakati wa uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji mifumo ya sekta za Umma
(PS3) mkoani Mwanza Aprili 27, 2016. Mradi huo unafadhiliwa na shirika la
Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) ni
wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 97
katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
PS3
inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha
mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu,
fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika
ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na
matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.
Pichani Kulia ni Kiongozi wa Utawala
na Ushirikishwaji wa Raia wa PS3, Dk. Peter Kilima.
Kiongozi
wa Utawala na Ushirikishwaji wa Raia wa PS3, Dk. Peter Kilima, akiwasilisha
mada wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwakilishi
kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bi. Beatice R. Kimoleta, akitoa neno wakati wa
uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Sehemu
ya washiriki waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza.
***********
Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Mwanza siku ya Jumatano na Alhamisi, Aprili 27-28, 2016. Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha
Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Watu takribani 180 walihudhuria. Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Dodoma, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri. Mkoa wa Mwanza una Halmashauri nane, ambazo ni: Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, na Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.
PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID. Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni: Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute. Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.
PS3 itaimarisha mifumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri. Mradi utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania. Mafanikio yanayotarajiwa ni pamoja na:
Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Raia: Uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga, kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta.
Rasilimali Watu: Kuongezeka kwa usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi. Kuimarisha mfumo wa ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini.
Fedha: Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza ufanisi katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.
Mifumo ya Mawasiliano: Kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini, pamoja na matumizi ya takwimu kwa wadau.
Utafiti Tendaji: Tafiti Tendaji muhimu zitakazosaidia mradi kujua changamoto na mikakati ya kuzishughulikia changamoto hizo. Tafiti hizi zitasaidia kugundua fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa. Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini.
0 comments:
Post a Comment