Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete (kati) akiongea na wanahabari jijini Arusha jana kuhusiana na Kampeni ya siku Kumi ya Usafi wa Mlima Kilimanjaro inayotarajiwa kuanza kesho. Wengine pichani ni Katibu Mtendaji wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania, Cyril Ako (kulia) na Mwakilishi kutoka Hoteli ya Kibo Palace, Jenipher Swai.
*******************
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) litazindua Kampeni Maalum ya siku 10 ya usafi
wa Mlima Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano ya TANAPA, Pascal Shelutete ilisema kuwa uzinduzi huo Utafanyika kesho Aprili 21,2016 na mgeni rasmi anataraji kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Said Mecky Sadik.
Kazi hiyo ya kusafisha Mlima
Kilimanjaro itafanywa na watumishi wa hifadhi kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa utalii zaidi ya 200, wakiwemo mawakala wa utalii (tour operators), waongoza wageni (guides),
wapagazi (porters) na wapishi (cooks) wanaowahudumia watalii katika Hifadhi ya
Taifa ya Kilimanjaro.
"Usafi huu utahusisha maeneo
mbalimbali ya hifadhi kama vile njia za kupandia mlimani, maeneo ya kupiga
kambi, maeneo ya mabanda, na maeneo ya kupumzikia wageni picnic sites,"alisema Shelutete.
Alisema kuwa kampeni hiyo ni muendelezo wa
utaratibu wa kawaida wa hifadhi unaofanyika kila wakati kuhakikisha maeneo ya
hifadhi hasa yanayotumika na wageni yanakuwa katika viwango vya kimataifa vya
utoaji huduma kwa wageni.
Shelutete alisema huo ni utaratibu wenye lengo la kuwahamasisha wadau
mbalimbali kuhakikisha kuwa wanauweka Mlima Kilimanjaro katika hali ya usafi
muda wote.
Mlima Kilimanjaro unachangia
zaidi ya Shilingi Bilioni 60 ambazo ni sawa na asilimia 34 kwa mwaka katika
mapato ya TANAPA. Aidha, Mlima Kilimanjaro hutoa ajira zaidi ya laki
tatu(300,000) kwa mwaka kwa Watanzania wanaofanya shughuli za utalii mlimani.
0 comments:
Post a Comment