Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba, (Kushoto), baada ya kuridhishwa na maelezo ya kina kuhusu huduma na kazi zifanywazo na Mfuko huo katika kutoa mafao ya muda mfupi na fidia ya kudumu kwa Wanyakazi wa Sekta Binafsi na Umma watakaopata ajali na kuumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wazifanyazo mwanzoni mwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa Tanzania (ALAT), ulioanza mjini Dodoma leo Aprili 8, 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto), akitoa ufafanuzi
kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Juu ya Huduma na Mafao yatakayotolewa na
Mfuko hususani fidia ya muda mfupi na fidia ya kudumu kwa Wanyakazi wa Sekta
Binafsi na Umma watakaopata ajali na kuumia, kuugua ama kufariki kutoka na
kazi. Awali Bw. Mshomba alipata fursa ya kutoa mada kwa wajumbe wa ALAT, kutoka
mikoa mbalimbali kuhusu huduma za Mfuko huo. Katikati ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI), Suleiman Jaffo.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba akiwasilisha mada
Baadhi ya wajumbe wa ALAT na wageni waalikwa
Baadhi ya wajumbe wa ALAT na wageni waalikwa
Mmoja wa wajumbe akizungumza kwenye mkutano huo
0 comments:
Post a Comment