Mama
Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akiwa na mwanae Mhe. Makongoro
Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari wakati walipotembelea Daraja la
Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam.
Mama
Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akiwa na mwanae Mhe. Makongoro
Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari wakati walipotembelea Daraja la
Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam.
Mama
Maria, ambae hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana mwenye furaha
kufika darajani hapo kwani ndoto ya miaka mingi iliyoanzishwa na hayati Baba
wa Taifa, Mwal Julius Nyerere imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John Pombe
Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina la Mwalimu na siyo yeye,
jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na nvijavyo
vitamkumbuka mwasisi wa Taifa.
********************
Mke wa
Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Maria Nyerere
ametembelea Daraja la Nyerere linalounganisha eneo la Kigambaoni na Kurasini
Jijini Dar es salaam na kuipongeza serikali na wananchi wote wa Tanzania kwa
kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo kubwa na la kisasa kwa nchi za Afrika ya
Mashariki na Kati.
Mama
Maria Nyerere aliyeongozana na Mwanae Mheshimiwa Makongoro Nyerere amesema
kukamilika kwa daraja hilo ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni
254.12 kumekamilisha mpango wa miaka mingi ulioanzishwa na Hayati Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa na nia ya kujenga daraja katika eneo
hilo la mkondo wa bahari lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti haikuwezekana.
Aidha,
Mama Maria Nyerere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kwa kuamua Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere kwa heshimu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere, na amebainisha kuwa uamuzi huo utaviwezesha vizazi
vijavyo kutambua juhudi zilizofanywa na mmewe katika ujenzi wa nchi.
"Mimi
ninamshukuru sana Rais kwa maana ilikuwa lipewe jina lake, lakini yeye Mungu
akamjaalia akasema kwamba hapana tukumbuke tulikotoka, kwa hiyo najisikia
vizuri sana, na familia nayo inajisikia vizuri sana, lakini zaidi na watanzania
wanajisikia vizuri sana, kwa maana watakuwa wanaulizana Nyerere alikuwa ni
nani?" Amesisitiza Mama Maria Nyerere.
Daraja
la Nyerere lenye urefu wa meta 680, upana wa meta 3.2, njia sita za magari na
barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 2.5, lilifunguliwa na Rais wa awamu
ya tano Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 19 Aprili, 2016 na linakuwa kiunganishi
muhimu kati ya Kigamboni na katikati ya Jiji la Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment