Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Sabasaba Moshingi, (wapili
kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jukwaa la Wahariri
Tanzania, (TEF), kutoka kushoto, Makamu mwenyekiti, Deodatus Balile,
Mwenyekiti, Theophil Makunga,
na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa TEF, baada ya kuwakabidhi tuzo za kutambua
mchango wa vyombo vya habari katika kuwaelimisha wananchi juu ya huduma
zitolewazo na benki hiyo kongwe hapa nchini na kwa kuchaguliwa kwao kuwa
viongozi wapya wa TEF. Tukio hili lilifanyika wakati wa hafla ya kila mwaka
inayoandaliwa na benki hiyo ya kukutana na wahariri kuzungumzia mafanikio na
changamoto za benki hiyo na malengo
iliyojiwekea mwaka huu.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan
Said
BENKI ya
Posta Tanzania, (TPB), imekutana na wahariri wa vyombo vya habari hapa
nchini, na uongozi mpya wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, na
kuelezea mafanikio ambayo Benki hiyo kongwe hapa nchini imeyapata
katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2016.
Pia Benki
hiyo imeeleza mkakati wake mpya wa kuifanya benki hiyo kuwa moja ya
mabenki makubwa kabisa sio tu hapa nchini bali nje ya mipaka ya nchi
ambapo sasa inatarajia kuwa na jengo lake la kisasa. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Akizungumza
kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Ijumaa usiku Machi
18, 2016, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi
alisema, mafanikio ya benki hiyo yanatokana na kuweza kuingiza makundi
mengi zaidi kufungua akaunti na kuwa na utamaduni wa kuweka akiba
ambapo kila uchao idadi ya wateja wapya inazidi
kuongezeka.Ramani ya Tanzania ikionyesha mtandao wa benki ya posta Tanzania, TPB |
Pia alisema, benki hiyo imeziti
kutanua mtandao wake kwa kuboresha muonekano wa matawi ya benki hiyo
katika mikoa 26 ya bara na visiwani. Alsiema sambamba na matawi hayo
huduma za kibenki zinapatikana kote nchini kwenye ofisi za
posta.
Makamu mwenyekiti wa TEF, Deo
Balile, (kulia), akipokea tuzo yake
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB,
Sabasaba Moshingi, (watatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers nchini, TBN, Joachim Mushi,
(wakwanza kulia), makamu Mwenyekiti wa TBN, Khadija Kalili, (wanne
kushoto), Mmiligi wa K-VIS MEDIA na K-VIS Blog, Khalfan Said,
(wakwanza kushoto) na Mhariri Mtendaji wa Business Times/Majira, Bw.
Imani (wapili kushoto)
Moshingi akitoa maelezo ya kina
kuhusu huduma za TPB, mafanikio iliyopata na malengo yake ya
baadaye
Wahariri wakiwa kwenye hafla
hiyo
Moshingi
akitoa maelezo ya kina kuhusu huduma za TPB, mafanikio iliyopata na
malengo yake ya baadaye
Deo Balile akizungumza kwenye
hafla hiyo
Mhariri Mtendaji wa gazeti la
The Guardian, Wallace Mauggo, akizungumza kwenye hafla
hiyo
Mhariri wa biashara wa gazeti la
Daily News, Henry Lyimo, akizungumza kwenye hafla hiyo
Mwenyekiti wa TBN, Joachim
Mushi, akizungumza kwenye hafla hiyo
Mwenyekiti wa Jukwaa la
wahariri, Theophil Makunga akizungumza
Mhariri Mtendaji wa EFM Radio,
Scholastica Mazula, akizungumza.
Meneja Mkuu anayeshughulikia masuala ya shirika, na mahusiano ya umma, wa TPB, Noves Moses, akizungumza kwenye hafla hiyo |
Mkurugenzi wa matekelezo na
udhibiti majanga, Moses Manyatta(aliyesimama),
akizungumza
Moses Nyenyembe, Mkurugenzi wa
Ukaguzi wa ndani
Mkurugenzi wa wateja na
biashara, Henry Bwogi
Mkurugenzi wa Teknolojia na
Operesheni wa TPB, Jema Msuya
Mkurugenzi wa masuala ya sheria
na katibu wa bodi ya TPB, Mystica Mapunda Ngongi
Manyerere Jackton, Mhariri wa
gazeti la Jamhuri
Picha ya pamoja
Afisa Mtendaji Mkuu, Sabasaba
Moshingi, akiteta jambo na Afisa wa mawasiliano wa TPB, Theo
Mwakifulefule
0 comments:
Post a Comment