Na: Frank Shija,
WHUSM
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewasimamisha kazi
watumishi wawili wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC kutokana na utendaji
usioridhisha.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika ofisi za TBC leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape
amewataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari
na Matukio Bwana Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi Bibi. Edna Rajab ambao
wote kwa pamoja wasimamishwa kazi na uamuzi huo utafikishwa kwa Bodi ya TBC kwa
hatua zaidi. “ Tunachukua
uamuzi wakuwasimamisha kazi watendaji hawa ili kujenga upya Idara hii muhimu
katika ustawi wa TBC na habari kwa ujumla” Alisema Nape
Aidha Waziri
huyo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuwachukulia hatua watumishi wengine
walio chini ya Idara hiyo kwakuwa wako chini ya mamlaka yake na kutoa mrejesho
wa hatua alizochukua dhidi ya wale wote wilioonyesha utendaji mbovu.
Alisema kuwa
Serikali imefikia uamuzi huo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu
juu ya utendaji mbovu na wakutoridhisha viongzi na baadhi ya watumishi wa Idara
hiyo hiyvo hatua hizo zimechukuliwa ikiwa ni
kujenga upya na kuboresha Idara hiyo muhimu katika uendeshaji wa Shirika
lolote lile la Habari na kuongeza ufanisi.
Idara ya Habari
na Matukio ya TBC inaundwa na Mkurugenzi wa Idara, Meneja wa Vipindi Wahariri
na Waandishi wa Habari ambapo tayari Mkurugenzi na Meneja wa Vipindi
wamesimamishwa kazi leo tarehe 15 Februari 2016 na watumishi wengine
watachukuliwa hatua kufuatia agizo la Mhe. Waziri wa Habari kwa Mkurugenzi Mkuu
wa TBC alilolitoa leo wakati akitangaza kuwasimamisha kazi viongozi hao.
0 comments:
Post a Comment