Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam
(DAWASCO), imesema imeweza kutekeleza mipango na maagizo mbalimbali
yaliyotolewa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John
Magufuli, hivyo kuwezesha kupunguza kero na kuboresha huduma ya Majisafi na
uboreshwaji wa Majitaka Jijini Dar es Salaam ndani ya siku 100 tangu Rais Dkt
Magufuli aingie madarakani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam kuhusu mafanikio yaliyopatikana ndani ya siku 100 za utawala wa
Rais Magufuli, Afisa mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja
ametaja mambo yaliyofanikiwa ni pamoja na Kufungua njia za Maji zilizofungwa
kutokana uchakavu wa miundo mbinu , Kuzuia mivujo mikubwa na midogo ,kuunganishia
wateja wapya huduma ya Maji, ufufuaji wa Mita kuu (Bulk meters),
uboreshaji wa mfumo wa malipo ,uboreshaji
wa migao ya Maji pamoja na uboreshaji wa huduma kwa wateja.
“Shirika limeweza kupeleka Maji katika maeneo mengi
zaidi ya jiji la Dar es Salaam ambayo hayakuwahi kupata Maji au huduma
ilisitishwa kwa sababu ya uchakavu wa miundo mbinu. Katika Kipindi hiki cha Mh.Rais
Dkt John Pombe Magufuli, jumla ya maeneo 52 yameweza kupata Maji kwenye wilaya
zote tatu za Kinondoni, Ilala na Temeke mfano maeneo ya Temeke sokota, Kimara B,
na Buguruni mnyamani na mengine mengi maana Rais aliagiza tumtue Mama ndoo kichwani”.
“Pia tumeendelea kutekeleza agizo la kufikisha wateja
milioni 1 ifikapo juni 2016 hivyo tumeanza kuunganisha wateja wapya na mpaka
sasa tumeweza kuunganisha wateja 3500, lakini mradi wa Ruvu chini unatarajia
kuisha Februari 2016 mwishoni na kuongeza upatikanaji wa Maji toka lita za
ujazo 300milioni mpaka lita 450 milioni hivyo sehemu ambazo hawajafikiwa na
huduma ya Maji wataweza kufikiwa”.
“kwa upande wa miradi kwa siku 100 za Mh Raisi Kuna
miradi miwili imeshakamilika ambapo ni Mradi wa Kibamba shule uliopo kibamba
ambapo unahudumia wananchi takribani na
Mbweni teta uliopo wilaya ya kinondoni ambao nao unahudumia wananchi takribani.
Pia tumeweza kupunguza upotevu wa Maji( Non Revenue
Water) kutoka asilimia 57 mwanzoni mwa mwezi September 2015 mpaka asilimia 42
kwa mwezi January 2016 na juhudi zinaendelea kupambana na upotevu wa Maji ili
tufikie lengo la chini ya asilimia 20 ifikapo 2018.
“Tumeweza
kuwabaini watumiaji maji 1250 walio nje ya utaratibu (informal Water users) ambao
ni watengeneza bustani, watengeneza matofali, hotel na lodge ambazo walikuwa
hawalipii huduma ya Maji na kuzisajili rasmi na sasa wana mita kabisa na
wanalipia huduma ya Maji kila mwezi hivyo kuongeza Mapato ya Shirika” aliongeza
Mhandisi Luhemeja wamekamatwa waliokuwa wanatumia Maji kiholela bila
kuunganishiwa na Dawasco”.
“Makusanyo yameongezeka ndani ya siku 100 Shirika
limeweza kuongeza mapato yake kutoka bilioni 4 mpaka bilioni 7 kwa mwezi pia tumeboresha kitengo cha huduma kwa wateja
na hivi sasa kinafanya kazi kwa muda wa masaa 24 na hivyo kutoa nafasi kubwa
kwa mteja kupata huduma muda wowote anapo pata tatizo au msaada” . Alisema Mhandisi Cyprian Luhemeja.
0 comments:
Post a Comment