Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame Mbarawa akiongea na Viongozi pamoja na Wafanyakazi wa TAZARA alipotembelea ili kutoa muongozo wa utendaji
kazi katika Shirika hilo.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi
na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelezeko ya utendaji
kwa Naibu Mkurugenzi wa TAZARA, Betram Kiswaga alipotembelea Ofisi za Shirika hilo leo jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Shirika la
TAZARA Wakimsikiliza Waziri Profesa Mbarawa Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.
**************
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame mbarawa amewataka watendaji na
wafanyakazi wote wa shirika la reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), kufanya
kazi kwa umoja,uwazi na uadilifu ili kufikia malengo yaliokusudiwa na kuhuisha
ustawi wa shirika hilo.
Akitoa
mwelekeo wa utendaji wa shirika hilo kwa watendaji na watumishi wa TAZARA Prof.
Mbarawa amesema Serikali ya awamu ya tano inaitaka TAZARA kufanya kazi kibiashara
kwa kuhudumia wasafiri na wasafirishaji kikamilifu ili kuinua uchumi wa shirika
hilo na kuliondolea unyonge na migogoro ya mara kwa mara.
“Acheni kufanyakazi kwa upendeleo na usiri kwani huo
ndio mwanzo wa hujuma na ubadhirifu hali inayochochea malalamiko na kudumaza TAZARA”,
amesema Prof. Mbarawa. TAARIFA ZAIDI BOFYA HAPA.
Amezungumzia
umuhimu wa kila mfanyakazi kufanya kazi kwa uadilifu na malengo ili kuleta
matokeo chanya kwa manufaa ya TAZARA na nchi wanachama.
Kuhusu
ubadhirifu unaotokea TAZARA Prof. Mbarawa uchunguzi wa TAKUKURU umeshaanza na kusisitiza kuwa hatua za kisheria
zitachukuliwa kwa wahalifu wote bila kujali wanatoka upande gani wa TAZARA.
Naibu Mkurugenzi wa TAZARA Bw, Betram Kiswaga
amemweleza Waziri kuwa TAZARA inakabiliwa na changamoto za kimtaji,kiufundi na
upungufu wa injini na mabehewa hivyo ameiomba serikali kuiwezesha ili imudu
kujiendesha.
Amemhakikishia
Waziri kuwa tayari shirika hilo limeanza kupata wasafirishaji wa uhakika hivyo
kuimarika kimtaji kutavutia wasafirishaji wengi zaidi.
Reli ya TAZARA
inayounganisha nchi za Tanzania na Zambia iliyojengwa na wachina miaka ya sabini na ina mtandao wa KM 1860 kutoka
Dar es Salaam hadi Kapirimposhi lengo likiwa ni kuimarisha biashara na uchukuzi
kati ya nchi hizo na kukuza uchumi.
Imetayarishwa
na Kitengo cha Habari, Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
0 comments:
Post a Comment