Elimu ya masuala la Jinsia
ambayo imekuwa ikitolewa kwa wafanyakazi wa makampuni tanzu ya TBL
group kwa wiki tatu mfululizo jana yaliwafikia wafanyakazi wa kampuni hiyo wa
kiwanda cha kutengeneza bia cha Mwanza.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL
Mwanza ambao walipata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo ambayo yameendeshwa na
Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni
Inspekta Prisca Komba wamesema yamewawezesha kuelewa masuala mbalimbali
yanayohusiana na jinsia.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni
Inspekta Prisca Komba akitoa mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha
TBL Mwanza .Mafunzo haya yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya
TBL Group nchini
Wafanyakazi wa TBL Mwanza wakimsikiliza Bi.Enid Muro,mmoja wa watoa
mada katika semina hiyo.
Meneja
Uhusiano wa kampuni ya kampuni ya TBL Group,Editha Mushi akiongea na
wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha Mwanza wakati wa semina ya masuala ya jinsia
iliyofanyika mkoani humo jana.Semina kuhusiana na masuala ya jinsia kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo imefanyika pia
kwenye viwanda vyake tanzu nchini kote na kuendeshwa na Mkaguzi Msaidizi wa
jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba
0 comments:
Post a Comment