JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
TAARIFA KWA
UMMA
KUFUNGWA KWA MUDA BARABARA YA MPANDA - KOGA -
TABORA
Tunapenda
kutoa taarifa kwa Umma kuwa, Barabara ya Mpanda - Koga - Tabora imefungwa kwa
muda kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini zilizosababisha kufurika
kwa mto Koga na kufanya daraja la Koga, lililopo mpakani mwa Mikoa ya Katavi na
Tabora kutopitika na hivyo kukata mawasiliano ya barabara katika mikoa hiyo.
Kutokana na
kukatika kwa mawasiliano ya barabara kupitia daraja hilo, tunaomba wananchi
kusitisha safari kwa kutumia barabara hiyo ili kuepusha madhara yanayoweza
kujitokeza hadi hapo barabara hiyo itakapofunguliwa mara tu baada ya maji
kupungua katika eneo hilo.
Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kifungu cha
41 (1) cha Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni ya 8 (1) ya Kanuni
za Usimamizi za Barabara za Mwaka 2009.
Wizara,
inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote.
Imetolewa na:
Eng. Joseph
Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)
28/01/2016
0 comments:
Post a Comment