Meneja
Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (kulia) na Afisa wa Airtel kitendo
cha huduma za Intaneti, Ndevonaeli Eliakimu kwa pomoja wakionyesha
bango la modemu mpya ya Airtel wingle wakati wa uzinduzi wa modemu mpya
itakayowawezesha wateja wake kufurahia huduma za Intaneti na Wi-Fi kwa
pamoja na kuunganisha zaidi ya vifaa 10 kwa wakati mmoja.
Meneja
Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (kushoto) akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa modemu mpya
itakayowawezesha wateja wake kufurahia huduma za Intaneti na Wi-Fi kwa
pamoja na kuunganisha zaidi ya vifaa 10 kwa wakati mmoja. Akishuhudia
ni Afisa wa Airtel kitendo cha huduma za Intaneti, Ndevonaeli Eliakimu
Afisa wa Airtel kitendo cha huduma za Intaneti, Ndevonaeli Eliakimu akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa modemu
mpya itakayowawezesha wateja wake kufurahia huduma za Intaneti na Wi-Fi
kwa pamoja na kuunganisha zaidi ya vifaa 10 kwa wakati mmoja.
Mwandishi
wa habari wa Star TV, Grace Semfuko akikabithiwa modemu yake ya Airtel
Wingle na Afisa wa Airtel kitendo cha huduma za Intaneti, Ndevonaeli
Eliakimu mara ya kuibuka mshindi katika raffle iliyoendeshwa wakati wa
uzinduzi. akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
**********
Kampuni
ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua modemu mpya ya maajabu
itakayowawezesha wateja wake kufurahia huduma za Intaneti na Wi-Fi kwa
kuunganisha vifaa zaidi ya 10 kwa wakati mmoja wakiwa mahali popote
nchini
Modemu
hiyo ya maajabu ijulikanayo kama “Airtel Wingle” imelenga kutatua
mahitaji ya huduma za kimtandao kwa watumiaji wake ambapo mahitaji ya
huduma za intaneti yamekua kwa kasi nchini na kuifanya Airtel kuleta
modem hiyo ya maajabu ili kuwahakikishia wateja wake uhakika wa huduma
za kimtandaoni kwa gharama nafuu zaidi nchi nzima
Akiongea
wakati wa halfa ya Uzinduzi iliyofanyika katika duka la Airtel Expo
lililopo jijini Dar es Saalam, Meneja Uhusiano wa Airtel , Bwn Jackson
Mmbando allisema “Tunayofuraha kuzindua modemu hii ya kipekee ya Airtel
wingle ambayo huduma zake zinaenda sambamba na dhamira yetu ya
kuwafikishia wateja wetu huduma za intaneti zenye kasi zaidi na pia
kuwaongezea wateja hao huduma nyingine bora zaidi za Wi-Fi kwa
kuwafaidisha wateja wengi kwa modem hiyo hiyo moja wakiwa mahali popote”
Eliakimu
alifafanua kuwa “Bila kujali mtandao unaotumia, modemu ya Airtel
Wingle itawawezesha wateja wetu kuunganisha zaidi ya vifaa au watumiaji
10 kwa wakati mmoja na kufaidi huduma ya Wi Fi kwa kasi na urahisi.
Modem hii ya maajabu yenye Wi-Fi itaweza kutumika na familia, marafiki
kwenye ofisini au popote mara tu inapounganishwa kwenye Laptop au katika
sehemu yeyote inayoweza kutumia Modem kama vile kwenye gari, soketi za
ndani ya nyumba au Hotelini, Televisheni pamoja vifaa vingine vingi
vinavyotumia modem”
Akiongea
kuhusu upatikanaji wa modemu hiyo, Afisa wa Airtel kitendo cha huduma
za Intaneti, Ndevonaeli Eliakimu alisema, Modem ya Airtel wingle inakuja
na ofa kabambe ya kifurushi cha Internet cha 5GB kwa mwezi. Tumejipanga
kuendelea kutoa huduma za kabambe zitakazowapatia wateja thamani ya
pesa zao. Modemu hii ya Airtel Wingle itapatikana katika maduka yote ya
Airtel nchi nzima na pia itapatikana katika Duka letu la Airtel Expo kwa
bei nafuu yaani OFA kuanzia sasa”
Airtel
imezinduzi modemu ya maajabu ya Airtel Wingle ikiwa ni muda mfupi tangu
ilipozindua duka lake la kisasa la Airtel Expo jijini Dar es salaam
ili kudhihirisha dhamira yake ya kutoa huduma za kisasa zenye ubunifu
unaoendana na karne ya sasa ya mawasiliano huku ikitoa huduma hizo kwa
gharama nafuu zaidi.
0 comments:
Post a Comment