Tarehe 23 Desemba,
2015 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliwateua
Mawaziri wanne, Naibu Waziri mmoja na kumhamisha Wizara Waziri mmoja.
Walioteuliwa ni
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge,
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt. Joyce Ndalichako na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Hamad Yusuf Masauni.
Rais Magufuli pia
alifanya uhamisho wa Waziri mmoja ambaye ni Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kutoka
Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.
Kufuatia
uteuzi huu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
anawaarifu Mawaziri wote na Naibu Waziri walioteuliwa kuwa wataapishwa Jumatatu
tarehe 28 Desemba, 2015 Saa tatu
asubuhi, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
24 Desemba,
2015
0 comments:
Post a Comment