Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George
Masaju (kulia) akiwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo wakati
wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya 104.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akizungumza
na Mawakili 104 walioapishwa leo jijini Dar es salaam. Mhe. Chande amewataka Mawakili
hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma yao.
Mawakili wakiwa wamesimama mbele ya
Jaji Mkuu kabla ya kuapishwa.
Mawakili walioapishwa wakiwa katika picha
ya pamoja na Jaji Mkuu Mhe. Othman Chande na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania.
*****************
Na Aron Msigwa –MAELEZO
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.
Othman Chande amewataka Mawakili kote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia
weledi na maadili ya taaluma ya Sheria na kwamba wasisite kuwaeleza ukweli
wateja wao wanaopeleka mashauri Mahakamani ili kuepuka kupoteza muda na gharama
katika masuala yanayoweza kupatiwa ufumbuzi nje ya Mahakama. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Akizungumza na Mawakili wapya
104 waliohitimu Shule ya Sheria kwa mwaka 2015 wakati wa hafla ya 53 ya
kuwapokea na kuwaapisha iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee leo jijini Dar
es salaam amesema kuwa msingi mkubwa wa kazi yao umejengwa katika uzingatiaji
wa maadili ya taaluma ya sheria.
Amewataka Mawakili hao
kubadilika kifikra kwa kuwa Mawakili Bora ili kujenga imani na uaminifu kwa
jamii wanayoihudumia na kuongeza kuwa sasa wameingia kwenye utaratibu wa
kutambuliwa rasmi na Mahakama ya Tanzania kwa kuwezeshwa kufanya shughuli za
uwakili kwenye mahakama ya Tanzania maeneo mbalimbali nchini.
“Naomba
mtambue kuwa kila Wakili ni Ofisa wa Mahakama hivyo mnao wajibu na jukumu la
kusoma, kufuatilia mashauri mbalimbali ili kuwa na uhakika wa kesi mnazosimamia
kuliko kuzitegemea Mahakama”
Aidha, ameeleza kuwa yapo
mambo ambayo yamekua yakifanywa na baadhi ya Mawakili wasio waaminifu
yanayochafua sura ya Taaluma ya Sheria ikiwemo kutumia nyaraka za kughushi,
kuvunja Kanuni na Maadili ya Taaluma huku baadhi yao wakijikuta wakiingia
katika mgogoro na Mamlaka zinazosimamia kitaaluma taaluma hiyo.
“Nawataka
mzingatie sheria, kanuni na Maadili ya Uwakili, hata hivyo tuna chombo
kinachosimamia maadili yenu, wapo takribani 176 waliokiuka maadili na hawa
wanashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria ili kulinda maadili na utendaji wa taluma
yenu”
Amesisitiza Mhe. Othman.
Amewataka watimize
wajibu wao kwanza kwa wananchi watakaouhudumia pamoja na Mahakama ya Tanzania
ambayo inawataka kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria, kanuni na
taratibu zilizowekwa.
Mhe. Othman amefafanua kuwa
Mahakama ya Tanzania inaendelea na Mkakati wa kupunguza mrundikano wa Kesi
Mahakamani kwa kuhakikisha kuwa kesi zote zinazofikishwa Mahakamani
zinamalizika katika kipindi cha chini ya mwaka 1
Ameeleza kuwa silimia 47 ya
kesi zaidi ya 200 zilizokuwepo Mahakama Kuu katika kipindi cha miaka 4
iliyopita zimeendelea kusisikilizwa kwa ubora na sasa zimebaki asilimia 17 ya
kesi hizo jambo linaonyesha kuongezeka kwa ufanisi wa Mahakama.
Kwa upande wake Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akiwakaribisha Mawakili hao katika familia
ya sheria Tanzania amesema kuwa katika jamii wanao mchango mkubwa katika
kuhakikisha Haki na Usawa vinadumishwa nchini.
Amesema mawakili hao kabla ya
kuapishwa na kuingizwa kwenye utaratibu wa kutambuliwa kuwa Mawakili wamepitia
na kufauru vigezo vya kitaaluma vilivyowekwa ili kulinda heshima ya Taaluma ya
sheria nchini.
Amewaeleza kuwa mara baada ya
kupokea viapo vyao wameingia kwenye utumishi wa umma kutekeleza majukumu yao ya
kikatiba na kuongeza kwamba wao kama wanasheria wanatakiwa kuzingatia weledi wa
taaluma yao.
Amewataka kuwa makini katika
utendaji wao kwa kuepuka kuwa sehemu ya migogoro na kuepuka kuegemea upande
wowote watakapokuwa wakitimiza majukumu yao ili kuendelea kujenga jamii ya
kistaarabu na ya kidemokrasia.
" Naomba mkumbuke kuwa
mna wajibu mkubwa kwa watu mtakaokuwa mnawahudumia, zingatieni maadili maana
ninyi sasa ni sehemu ya Mahakama ya Tanzania, fanyeni kazi kwa weledi na
umakini mkubwa" Amesisitiza.
Amesema utekelezaji wa majuku
yao ya kila siku ni sehemu ya utumishi wao katika umma hivyo wasiruhusu aina
yoyote ya ukiukwaji wa maadili yakitika kutimiza majukumu yao na kuwasaidia
wananchi wasiokuwa na kipato/ wananchi masikini watakakao omba msaada wao wa
kisheria.
Aidha amewataka wawe wabunifu,
kufanya kazi kwa bidii na kujiendeleza pale inapowezekana ili waweze kuwa
msaada kwa wananchi walio na kiu ya kupata huduma kutoka kwao.
Kwa upande wake Rais wa Chama
cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Charles Rwechungura akizungumza wakati wa wa
kuwakaribisha mawakili hao 134 amesema kuwa wao kama Chama cha Wanasheria
wanayofuraha ya kuwakaribisha wanachama wapya kwenye uwanja wa Sheria nchini.
Amesema mawakili hao wameingia
katika wakati muafaka kuongeza nguvu katika kuwahudumia wananchi huku akieleza
kuwa shule ya Wanasheria Tanzania itaendelea kutoa mafunzo na kusimamia viwango
vya taaluma ya sheria nchini na kuwataka mawakili hao kulinda heshima ya
taaluma ya sheria kwa kutoa huduma bora kwa umma.
0 comments:
Post a Comment