Nafasi Ya Matangazo

December 04, 2015


Mkuu wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Huawei, Jimmy Jin akizungumza na waandishi wa habari wa Tanzania na China wakati wa mkutano na waandishi hao uliofanyika Makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki wenye malengo ya kuweka mahusiano mazuri na kati ya waandishi wa habari na Kampuni hiyo.



 Kampuni ya Huawei Tanzania leo hii imewakaribisha waandishi wa habari mbalimbali jijini Dar Es Salaam kupata chai ya asubuhi pamoja na mkutano mfupi kuelezea mafanikio yake na mipango yake katika tasnia ya uandishi wa habari. Mkutano huu umefanyika katika ofisi za Huawei zilizoko Golden Jubilee Towers jijini Dar Es Salaam.



Mkutano huu uliwakutanisha waandishi wa Habari wa Tanzania na waandishi wa Habari raia wa China walioko Dar Es Salaam, hii ni kupitia muungano wa Wanahabari na Huawei ujulikanao kama Huawei Media Club. Muungano huu una lengo la kujenga mahusiano ya muda mrefu baina ya kampuni ya Huawei Tanzania na waandishi wa habari, pia kuendeleza mpango wa kampuni ya Huawei Tanzania kuendeleza sekta ya Teknolojia ya mawasiliano (IT) hapa nchini. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
 Akizungumza katika mkutano huu, Bwana Jimmy Jin, Meneja wa Habari wa Kampuni ya Huawei Tanzania aliitambulisha kampuni ya Huawei kama kampuni inayowajibika vema, yenye lengo la kuchochea ubunifu, kushirikiana na serikali kuwezesha sekta ya Teknolojia ya mawasiliano (IT) nchini Tanzania. Aliwakaribisha wanahabari na kusisitiza mawasiliano baina ya Huawei Tanzania na wanahabari katika mipango tofauti ya kuendeleza sekta ya Habari hapa nchini.
Bwana Jimmy alisema kwa mwaka 2015 Huawei Tanzania imekuwa na mafanikio makubwa mbalimbali hasa mwanzoni mwa mwaka huu ilipopokea cheti cha shukrani kutoka kwa Raisi Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na pia shukrani maalum kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda.

Aliendelea kusema kwamba mapema mwaka huu kuanzia tarehe 13 hadi tarehe 15 August Huawei Tanzania ilidhamini mkutano wa Raia wa Tanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) uliofanyika kwa mafanikio makubwa jijini Dar Es Salaam.

Alisema pia Huawei Tanzania iliandaa maonyesho maalum tarehe 18 June yaliyofahamika kama Huawei Cloud Conference (HCC) ambapo Huawei na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia walisaini mkataba ambao unaifanya Huawei kuwa mshauri wa serikali katika masuala ya sekta ya ICT. Katika mkutano huu serikali iliipongeza sana kampuni ya Huawei kwa uongozi mzuri na mchango wake mkubwa katika masuala ya ICT hapa nchini.

Bwana Jimmy aliendelea kusema kwamba mkutano huu ni miongoni mwa mikutano mingi ambayo Huawei itafanya, alisisitiza uwepo wa uhusiano mzuri kati ya wanahabari wa Tanzania na wanahabari wa China katika kipindi hiki ambacho uhusiano wa nchi hizi mbili unaendelea kukua vizuri siku hadi siku.


Posted by MROKI On Friday, December 04, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo