Nafasi Ya Matangazo

December 21, 2015

Inline image 1
MKALI wa miondoko ya R&B nchini Tanzania Ben Pol ameachia video yake ya wimbo ambao uko mtaani una bamba ile mbaya wa 'NINGEFANYAJE'.

Wimbo huo amewashirikisha wasanii mbali mvbali wa ndani na nje ya nvchi akiwepo, Avril Nyambura na mtanzania Rossie M

Ngoma hiyo kali imefanyiwa kazi na mwaandaaji wa muziki mahiri  Mswaki.

​Video ya NINGEFANYAJE imefanyika kazi nchini Afrika Kusini katika mji ule wa Pretoria, chini ya muongozaji maarufu wa mziki  Justin Campos kupitia kampuni yake ya  Gorilla Films.

NINGEFANYAJE ni video yenye historia ya halisi ambayo ilipata kumtokea rafiki wa karibu na Ben Pol. ni wimbo wenye hisia kali,"Nimeamua kusonga mbele' licha ya kuwa alikuwa amedatishwa vibaya na mahaba ya mpenzi wake. Pia wimbo unaelezea namna gani anaweza kuishi bila ya huyo msichana aliyempenda.
Tazama hapa   ‘NINGEFANYAJE’ ya Ben Pol
Posted by MROKI On Monday, December 21, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo