Mwanamuziki Ali Kiba
akionyesha machachari yake katika onyesho la Coke studio akiwa na mwanamuziki
wa Kenya Victoria Kimani
************
Mwanamuziki nguli wa miondoko
ya Bongo Fleva nchini Ali Kiba amesema moja ya mafanikio anayojivunia nayo
katika kazi ya muziki kwa mwaka huu ni ushiriki wake katika onyesho la Coke
Studio msimu wa tatu.
Ali Kiba ambaye amefanya
kolabo kwa kushirikiana na mwanamuziki wa kike anayetamba katika anga ya muziki
wa Bongo Fleva nchini Kenya Victoria Kimani amesema katika mahojiano hivi
karibuni kuwa anajivunia kuwa miongoni mwa wanamuziki wanaoshiriki kwenye msimu
wa tatu wa Coke Studio unaoendela ambapo kwa
hapa nchini onyesho hilo linarushwa na luninga ya Clouds kila Jumamosi saa 12
jioni na kurudiwa saa tatu usiku.
Anasema ushiriki wake kwenye
ni bonge la mafanikio kwani rekodi yake imezidi kuongezeka katika anga la
kimataifa na ameweza kujiongezea washabiki ambao wafuatilia onyesho hili
kupitia luninga,vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Mbali na kuongelea mafanikio
ya kupata washabiki amesema kuwa amefurahi kufanya kolabo (mash-up) na msanii
wa nje ya nchi kwa kuwa ameweza kujifunza mengi kupitia ushiriki wake kwenye
Coke Studio.
Alisema onyesho la Coke Studio
linadhihirisha kuwa muziki wa Bongo Fleva unazidi kukua na kuwa maarufu sehemu
mbalimbali barani Afrika kutokana na jinsi linavyofuatiliwa na idadi kubwa ya
watu hususani vijana.
Aliwataka wanamuziki wachanga
wanaochipukia kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanapata mafanikio.
“Fani ya muziki inazidi kukua
kiasi kwamba wakati wa kufanya muziki wa ndani tu imekwisha na inabidi kuvuka
mipaka na kufanya kolabo(mash-up) kama hizi za Coke Studio zinasaidia kupata
uzoefu na kufungua milango ya mafanikio”.Alisema.
Alimalizia kwa kuwapongeza
wanamuziki wenzake kutoka Tanzania ambao wako nao katika msimu wa Coke Studio
mwaka huu. Wanamuziki hao ni Ben Pol ambaye amefanya kolabo (mash-up) na
Wangechi kutoka Kenya, Fid Q ambaye amefanya kolabo (mash-up)Maurice Kirya na
Vanessa Mdee ambaye amefanya kolabo (mash-up) na mwanamuziki 2face kutoka
Nigeria.
Onyesho la Coke Studio
linarushwa na luninga ya Clouds kila Jumamosi saa 12 jioni na kurudiwa saa 3
usiku. Pia unaweza sikiliza show kwenye redio ya Clouds FM kila jumamosi saa 4
asubuhi.
0 comments:
Post a Comment