Nafasi Ya Matangazo

November 17, 2015



MISS Earth Tanzania 2008 ambaye kwa sasa ni Mwanamitindo wa Kimataifa, Miriam Odemba nimiongoni mwa majaji watakao jaji shindano la Miss Universe Tanzania 2015.

Majaji wengine watakaoshiriki katika kumtafuta mnyange wa mwaka huu ni Sheria Ngowi, Maria Sarungi Tsehai, Mariam Ndaba na Priyal Lavin’ia.

“Maandalizi ya fainali ya shindano la Miss Universe Tanzania 2015 bado yanaendelea Mwanamitindo wa Kimataifa Miriam Odemba atakuwa jaji maalum katika kinyang’anyiro hiki cha kumpata mrembo wa Miss Universe Tanzania 2015,”alisema msemaji wa Compass Communication, Hamid Kad.

Kadi amesema zoezi la usaili limeshakamilika na hatimaye kupata warembo watakaojiunga na kambi ya Miss Universe kesho siku ya jumatano kabla ya fainali tarehe 20 mwezi huu.

Amewataja warembo waliobahatika kuingia kambini ni 14 tu, majina na mikoa waliyotoka kwenye mabano Mariam Isack (Dar es salaam), Lilian Luth(Dar es salaam), Stacey Sulul(Dar es salaam),Willice Donard(Dar es salaam), Lorraine Marriot(Dar es salaam), Dalena David(Dar es salaam), Mercy Zephania(Dar es salaam), Dinnah Kaijage(Dar es salaam), Melody Typhone(Dar es salaam), Joselyn Mirashi(Arusha), Nancy Matta(Mbeya), Christina Shimba(Iringa), Belinda (Mwanza).

 Mwaka huu Miss Universe imefanya usaili katika mikoa sita tofauti ikiwamo Tanga, Iringa, Mbeya, Arusha, Mwanza na Dar es salaam.


Miss Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuwapa warembo ili kujitambua kama vijana na kama wanawake hususani katika ujasiriamali. Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali toka katika Nyanja tofauti.

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ndio Mkurugenzi na Muandaaji mkuu wa Kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai amesema kuwa tofauti na miaka ya nyuma mwaka huu kambi itakuwa kwa muda mfupi zaidi kutokana na bajeti kuwa finyu. Halikadhalika usaili wa mwaka huu umefanyika katika mikoa sita.

 Kambi ya Miss Universe Tanzania 2015 imekamilishwa na warembo 16 kutoka mikoa sita ya Tanzania ambayo ni Arusha , Mwanza, Mbeya, Iringa,Tanga na Dar es Salaam.

Mashindano ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa Taifa bali pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 2008 Miss Universe Tanzania iliwakilishwa na Amanda Ole Sulul,2009 Illuminata James ,2010 Hellen Dausen  , 2011 Nelly Kamwelu, 2012 Winfrida Dominique,2013 Betty Boniface, 2014 Caroline Bernard ambaye ndiye anakabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.

Mashindano ya Miss Universe Tanzania imedhaniwa na   Compas Communications na New York Film Academy.
 

Fainali za mwaka huu za Dunia ambazo ni za 64 za Miss Universe 2015 zinataraji kufanyika katika mji wa Lass Vegas Marekani.

Mrembo Nale Boniphace ndio anashikilia taji la Miss Universe Tanzania alilolitwaa 2014.
Posted by MROKI On Tuesday, November 17, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo