Nafasi Ya Matangazo

September 28, 2015

Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akiangalia bidhaa aliyopokea kutoka kwa Marius Mutashobelwa  mkazi wa Mbeya, ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na Airtel FURSA walipotembelea ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya kuendeleza biashara zao mwishoni mwa wiki hii.
Mhandisi wa Airtel Gabriel Mshiu akiongea na vijana 13 waliowezeshwa na Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA walipotembelea ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya kuendeleza biashara zao mwishoni mwa wiki hii.
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea na vijana 13 waliowezeshwa na Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA walipotembelea ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya kuendeleza biashara zao mwishoni mwa wiki hii.Akishuhudia ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano (katikati) and  (kushoto) Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi.
 ***************
Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa kupitia mradi wake wa  Airtel FURSA imewakaribisha vijana wajasiriamali 13 katika Makao makuu yake yaliyopo Morocco na kujifunza uendeshwaji wa shughuli zake na kupatiwa mafunzo zaidi ya kibiashara kwa muda wa siku tatu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Meneja uhusiana na huduma kwa jamii  wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akizungumzia hilo alisema, “Airtel kwa kupitia mradi wake wa Airtel FURSA imeendelea kuwa mstari wa mbele kushirikiana na vijana katika kutatua changamoto wanazozipata katika kujikwamua kiuchumi. 

Alisema, “Tunayofuraha kuwakaribisha vijana wetu 13 tuliowawezesha katika biashara zao nakujikwamuakiuchumi kwa kuwapa nyenzo za kisasa zinazosaidia kukuza biashara zao na kujiongezea mapato. Pia ndani ya siku tatu wameweza kupatiwa mafunzo zaidi yatakayo wafanya waweze kuendesha biashara zao kwa njia ya kisasa na kuona ni jinsi gani wanaweza kuboresha biashara zao”

Pia walifanikiwa kukutana na Meneja wa Airtel Tanzania Bwana. Sunil Colaso na kumuelezea mafanikio waliyopata katokana na kuwezeshwa na Airtel FURSA. 

Bwana Sunil Colaso aliwaasa kutumia nafasi waliopata kujiendeleza katika biashara zao na Airtel iko pamoja na vijana ili kuhakikisha malengo yao yanatimia.

Iddi Chilumba mwakilishi wa vijana hao alisema, “Airtel FURSA ilinikuta nikiwa na nauwezo wa kubanjua korosho chache kutokana na vifaa duni, ila toka nimewezeshwa kwa mashine za kisasa na usafiri, sasa nabanjua korosho nyingi na kusafirisha kwenye masoko mbalimbali kwa haraka Zaidi. Nawashukuru sana Airtel kwa fursa walionipa na nawahasa vijana wenzangu wajishughulishe kuliko kukaa kijiweni na kujishughulisha na vitendo viovu”.

“Tunafurahishwa sana na juhudi zinazofanywa na vijana za kujitafutia maendeleo kwa njia zilizo halali na tuko tayari kushirikiana nanyi katika kutatua changamoto mnazozipata kwa kupitia mradi wa Airtel FURSA” alisema bwana Sunil Colaso.
Posted by MROKI On Monday, September 28, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo