Mratibu wa Veta kanda ya Dar es Salaam Bi. Frorence Kapinga akiwakaribisha wakuu wa vyuo vya ufundi vyenye usajili wa awali wa VETA kanda ya Dar es Salaam kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam. Bw.Habibu Bukko akizungumza jambo wakati wa mkutano la wakuu wa vyuo vya ufundi pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa kutano huo.
Mgeni rasmi Mwalimu Charles Philemon akizungumza na wakuu wa vyuo na wawakirishi wao(hawapo pichani) wakati alipokuwa anafungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi jijini Dar
Bw. Asanterabi Kanza ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA kanda ya Mashariki akiwasilisha mada kwa wakuu wa vyuo pamoja na wawakilishi wao(hawapo pichani) waliofika kwenye mkutano huo ili kukumbushana mmbo ya msingi kwenye uendeshaji wa vyuo hivyo vya ufundi.
Mkutano ukiendelea
Wakuu wa vyuo wakifuatilia kwa umakini kinachoendelea kwenye mkutano huo
Picha ya Pamoja
Na Mwandishi wetu
Kongamano la wakuu wa vyuo
pamoja na wamiliki wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya Dar es Salaam lafanyika
jijini Dar es Salaam kwa ajiri ya kupeana maelekezo kwa vyuo vilivyo pata
usajiri wa awali ili waweze kupata usajiri wa kudumu vilevile kupewa
hisibati na namna gani waweze kufuata taratibu ili kupata usajiri huo wa
kudumu.
Mwenyekiti wa bodi ya VETA
kanda ya Dar es Salaam Mwalimu Charles Philemon akiongea na wamiliki
na wakuu wa vyuo vya ufundistadi kuhusiana na wamiliki hao kupata usajili wa
kudumu kwani wao kama VETA familia wanauhitaji wa kutambua na haki ya kupata
hisibati inayoonyesha aina ya kozi zinazotolewa na chuo husika kilichopo
katika mfumo wa VETA, pia alisema wana mambo
muhimu ambayo yanayopaswa kukumbushana ni pamoja na wanayotekeleza,
kwani wao nia yao ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi kwa uhakika ili wao
waweze kuwa mabalozi wazuri katika kazi zao wawapo nje , tuendelee kujenga mambo
ya stadi za kazi katika vyuo vyetu ili kuwahakikishia wananchi kuwa tunaendelea
kutoa wakufunzi wenye sifa zinazostahili lakini yote haya yanatokana na kuwa na
chuo chenye usajili wa uhakika na wakufuata taratibu za mamlaka ya VETA.
Kwani watu mbalimbali hupimwa
kutokana na stadi zao mbalimbali wanazozipata katika vyuo vyetu na
kwenda nazo katika kuzitekeleza maeneo tofauti , watu hao ambao
wamepita kupitia katika mafunzo ya ufundi stadi VETA ndio watu
wenye stadi za kazi kwani hutenda kazi kutokana
na elimu na utashi mkubwa wanaoupata katika mafunzo yao
kupitia vyuo mbalimbali vyenye usajili wa VETA. anasema “kutokana na
semina zinazoendelea najua sisi ni familia moja hata kama katika familia kuna
watoto warefu na wengine wafupi lakini wote ni watoto wa VETA tufanye kazi kwa
umoja ili kutoa vitu vilivyobora zaidi kutofautisha na aina nyingize za utoaji
mafunzo, kwani ninaamini walimu wenye ubora ndio wanaopatikana katika mamlaka
ya VETA”
Pia aliweza kusisitiza fursa
ya kujengana kwa kutembeleana baina ya chuo kimoja na chuo kingine kwa ajiri ya
kupata ufanisi zaidi katika mafunzo mbalimbali pamoja na fani kwani
familia inajengwa kwa kuwa na uhusiano mzuri na uzuri wa familia huonekana
ndani ya VETA ni pale watu mnavyofaidika katika mambo mbalimbali iwe kwa
kujengana na kusaidiana kwa kuinua kile kinacho patikana kwani muda
mwingi huwa tunakutana mara moja katika maonesho mbalimbali lakini
familia hii ya VETA ni mamlaka inayo unganisha vyuo mbalimbali.
Naye mkurugenzi wa VETA
kanda ya Dar es Salaam Bwana Habibu Bukko alisisitiza kuhusiana na kusajiliwa
pamoja na kupata Hisibati itakayo saidia katika vyuo vyetu, hivyo aliweza
kusema baada ya kupata usajili ndani ya miezi kumi na mbili (12) ni lazima kila
chuo kiwe kimepata hisibati kwa wale wote waliokamilisha usajili huo wa mafunzo
ya ufundi stadi, pia aliweza kuzungumzia nini maana ya ambapo alisema HISIBATI
ni kutambua zile fani ambazo zinatolewa na chuo au umahili wachuo chako upo
kwenye fani zipi
0 comments:
Post a Comment